BYABATO AWASHIKA MKONO WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU

   

……………………………………………………………………………………..
Na Allawi Kaboyo – Bukoba
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na  Naibu waziri wa Nishati Advocate Stephen Byabato ametekeleza ahadi yake ya kusaidia Watoto ishirini Vifaa vya Shule kila Kata kwa Kata 14 za manispaa ya Bukoba, ahadi aliyoitoa siku Chache baada ya kupata wadhifa wa Naibu Waziri wa Nishati.
Watoto hao 280 wanaoishi katika familia Duni na wale ambao walishaondokewa na Wazazi wao (Yatima), wamepatiwa msaada huo wa sare za Shule, huku madaftali na kalamu vikitolewa na Diwani wa Kata ya Hamugembe Muhaji Kachwamba ili kupunguza makali ya gharama za Elimu.
Akizungumza kwa hisia wakati wa shukrani kwa Niaba ya wenzake mbele ya ugeni wa Mhe. Mbunge Byabato,  Mwanafunzi  Shaniat Amir ameshukuru Mhe. Byabato kwa wazo lake la kuwakumbuka Watoto hao na kuwachangia kidogo hicho.
Mwanafunzi huyo ameongeza kuwa licha ya kuwa serikali ya Rais. Dkt. John Pombe Magufuli inawasomesha bure, changamoto ya vifaa vya kujifunzia kwamaana ya madaftari na kalamu ilikuwa ikiwasumbua, hivyo msaada walioupokea utakuwa Chachu ya mafanikio Yao kielimu.
Mhe Stephen Amesema sare hizi zimetolewa kwa wanaostahili kupewa mahitaji hayo ikiwa Ni Mchakato iliyofanywa na Madiwani wa kata husika kwa Kushirikiana na TASAF pamoja na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Bukoba, na kuongeza kuwa huu ni mwanzo wa kutekeleza shughuli zilizopo kwenye Ilani na ambazo hazipo katika Ilani.
MAELEZO YA PICHA.
Sare na kalamu na Daftali zilizotolewa na Mhe. Mbunge Jimbo la Bukoba Mjini Advocate Byabato pamoja na Diwani Kata Hamugembe Muhaji Kachwamba kuwasaidia Watoto wanaoishi Mazingira magumu.
Mbunge Adv. Stephen Byabato akikabidhi sare za shule kwa moja kati ya Watoto wanaoishi Kata Hamugembe katika Mazingira magumu, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa.
Muonekano wa Watoto wa Kata Hamugembe wakiwa wamependeza ndani ya sare zao Mpya baada ya kukabidhiwa sare hizo na Mbunge Byabato.

Post a Comment

Previous Post Next Post