WATUMISHI WATATU WA TBS WASHIKILIWA KWA KOSA LA KUMTAPELI MMILIKI WA KIWANDA

  

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Katikati) akizungumza leo na wandishi wa habari makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.

***********************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe, ameiagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa shirika hilo kupisha uchunguzi baada ya kujihusisha na utapeli katika kiwanda cha Smart industries Limited kilichopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mhe.Kigahe ameitaka TBS kuchukua hatua za kinidhamu kwa watuhumiwa hao kulingana na taratibu na sheria za mtumishi wakati kesi hiyo inaendeshwa na TAKUKURU pamoja na jeshi la polisi.

“Mtumishi mmoja wa TBS ambaye anaitwa Suleimani Banza alienda katika kiwanda cha Smart industries Limited kilichopo maeneo ya Kijitonyama akiwa na lengo la kukagua bidhaa ambazo zimepitwa na muda lakini kutokana na kazi zake yeye si mkaguzi bali ni mtu wa kuweka viwango hivyo aliingilia jukumu sio la kwake”. Amesema Mhe.Kigahe.

Aidha Mhe.Kigahe amesema kuwa inasemekana mtuhumiwa huyo aliambatana na watu walioaminika ni maafisa polisi wakiongozwa na yeye wakiwa na gari la shirika la TBS kuingia kwenye ukaguzi huo ambao viongozi wa shirika walikuwa hawana taarifa nao.

“Watu hao walivyoingia katika kiwanda hicho waliweza kumtishia mwenye kiwanda kwamba anazalisha bidhaa kwa kutumia malighafi zizilizopitwa na wakati kwahiyo ili waweze kutokumfungia kiwanda chake anatakiwa awape fedha Milioni 100”. Amesema Mhe Kigahe.

Pamoja na hayo Mhe.Kigahe amesema Wizara ya Viwanda iliwachukua watuhumiwa watatu na kuweza kuwahoji ambao ni Afisa Viwango Suleiman Banza, Dereva ambaye alitumika kwenda katika kiwanda hicho Issa Mbaruku Dodo, Afisa Usafirishaji Thomas Elisha Mwankinga ambaye anatuhumiwa kutoa hilo gari kwenda kutumika katika tuhuma hizo.

Post a Comment

Previous Post Next Post