DKT NCHIMBI ATANGAZA NEEMA SINGIDA

 

MkuuwaMkoa wa Singida Dtk. RehemaNchimbi katikati akiongoza Kongamano
la Fursa za Uwekezaj ikwenye Mkoa wa Singida, Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida
Lucy Sheen,
kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi.

Wakuu  waWilaya zaMkoawaSingida(kwenye mstari wa kwanza)
wakifuatilia Mada mbalimbali wakati wa Kongamano la uwekezaji Mkoani Singida.

AfisaUhamasishaji Uwekezaji Mkuu kutoka Kituo cha
Uwekezaji nchini, Joyce Shundu akiwasilisha mada ya
Mazingira na Fursa za Uwekezaji Nchini”amepongeza jitihada na mikakati mbalimbali inayofanywa na MkoawaSingida

Viongozi
wa Wachimbaji Madini Mkoa wa Singida wakiwa kwenye banda lao
wakionyesha madini mbalimbali kwa wadau waliotembelea banda  la wachimbaji wa madini Mkoa wa Singida (SIREMA).


Wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakionyesha bidhaa zao

  • RAS ASEMA MKOA UMEJIANDAA KIKAMILIFU

 

Na John Mapepele, Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe,
Dkt. Rehema Nchimbi  amewataka  Wawekezaji kutoka  sehemu mbalimbali duniani kuja  kuwekeza 
kwenye  Mkoa wa Singida kwa
kuwa  Mkoa huo umebarikiwa kuwa na  fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo bado
hazijatumika kikamilifu.

Akifungua Kongamano la Mwongozo
wa Uwekezaji kwenye Mkoa wa Singida 
kabla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo huo, Dkt. Nchimbi amesema  Mkoa wa Singida  ni miongoni mwa  mikoa michache nchini  ambayo 
endapo fursa  zake zikitumika
utachangia  katika maendeleo ya Mkoa na
nchi kwa ujumla

Amezitaja baadhi ya fursa
zilizopo kwenye  Mkoa wa Singida kuwa
ni  pamoja na nishati ya mafuta asilia na
gesi, madini, kilimo cha alizeti,  korosho,utalii,
ufugaji wa nyuki na  kuku pia uwekezaji
kwenye sekta ya michezo ambapo amesema ni zamu ya Mkoa wa Singida  kuchangia 
kikamilifu kwenye uchumi wa nchi. 

Akitoa  mada kuhusu Uwekezaji wa  Alizeti mkoani Singida,
Mratibu wa Utafiti wa Alizeti nchini, Frank  Reuben  amesema zao la alizeti ndiyo zao pekee

linaloweza kuuvusha  mkoa  wa Singida 
kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa 
mkoa wa Singida  ndiyo unaongoza
hapa nchini kwa  kulima zao hilo.

Ametaja  baadhi ya  maeneo ya fursa za uwekezaji kwenye kilimo cha
Alizeti kuwa ni pamoja na uzalishaji na usambazaji wa mbegu, Kilimo bora
(mesto) cha alizeti na ufugaji nyuki (Agro-apiculture) na uendelezaji wa
viwanda vya kuchakata alizeti, chakula cha mifugo na mazao ya nyuki

Mtafiti wa zao la Korosho, kutoka
Taasisi ya Utafiti wa mazao ya Kilimo (TARI) Dkt. Fortunatus Kapinga  akitoa mada ya zao la Korosho nchini
amesema  Mkoa wa Singida una ardhi nzuri
yenye rutuba ambayo inafaa sana kwa zao la korosho  ukilinganisha na mikoa mingine  hapa nchini hivyo ni fursa pekee kwa  wawekezaji kuja  kufanya uwekezaji katika mkoa huu.

Amezitaja  baadhi ya bidhaa zinazopatikana kwenye zao la
Korosho kuwa ni pamoja na juisi, jamu,mvinyo, maziwa na siagi ambapo amesema
kauli mbiu ya mkoa kwenye uwekezaji kwamba  
“ni zamu yetu” ikitafsiriwa kwa vitendo italeta mageuzi makubwa  katika mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wanawake wachimbaji
Madini Mkoa wa Singida, Martha  Kayaga
amepongeza Serikali ya awamu ya Tano inayoongizwa  na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa
jitihada kubwa  inayofanya  kuwashilikisha  wachimbaji wazawa kwenye sekta ambapo
ameiomba Serikali kuangalia namna bora ambayo itawawezesha wajimbaji wadogo
wadogo kupata  mitaji hususan  vifaa ili waweze  kuongeza tija katika sekta  hiyo.

Pia Bi. Kayaga ameiomba
Serikali  kuwaangalia wachimbaji wanawake
kwa jicho la pekee kwa kuwa  wao  ni nguzo muhimu kwenye familia na kwamba
asilimia 10 inayotengwa kwenye Halmashauri imekuwa ikielekezwa kwenye sekta nyingine
ambapo amesisitiza endapo itaelekezwa kwa akina mama wachimbaji wadogowadogo
itasaidia kuinua hali za uchumi kuanzia kwenye ngazi ya kaya na Taifa kwa
ujumla.

Kwa upande wake, Afisa  Uhamasishaji Uwekezaji  Mkuu kutoka 
Kituo cha Uwekezaji nchini, Joyce Shundu 
akiwasilisha  mada ya “Mazingira
na Fursa za Uwekezaji Nchini”
  amepongeza 

jitihada na mikakati mbalimbali inayofanywa na Mkoa wa Singida kwa
kwenye uwekezaji  na kutoa wito kwa
wawekezaji kuwahi kuwekeza kwenye  fursa
za kipekee zinazopatikana mkoani hapa.

Awali katika salamu za
utambulisho, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi amewataka
Watendaji wote wa Serikali Mkoa wa Singida kuhakikisha wanajituma kufanya kazi
kwa weledi kwenye utoaji huduma  bora kwa
wawekezaji ili azma ya Serikali ya kutaka uwekezaji wenye tija itimie na
maisha  bora kwa watanzania ifikiwe.

Dkt. Lutambi amesema Serikali ya
Mkoa imeshaandaa mazingira wezeshi kwa 
wadau na wawekezaji makini kuja kuwekeza 
kwa kuzingatia sheria  na taratibu
za nchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post