Oktoba 23, 2020 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akiambatana na Meneja Utawala na Rasilimaliwatu wa Tume ya Madini, Gift Kilimwomeshi wameendelea na ziara katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma.
Mara baada ya kupokelewa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma na kutatua changamoto mbalimbali za kiutumishi pamoja na kutoa miongozo mbalimbali ya kiutumishi wametembelea Mgodi wa Makaa ya Mawe na Ngaka.