…………………………………………………………………………………….
NJOMBE
Serikali ya Tanzania imetenga zaidi ya bil 200 zinazofadhiriwa na serikali ya India kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa miradi mikubwa ya maji itakayomaliza tatizo la muda mrefu la huduma hiyo kwa wakazi wa miji ya Njombe ,Makambako na Wanging’ombe mkoani Njombe
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa yenye vyanzo vingi vya maji ambavyo havitumiki ipasavyo ambapo hadi sasa inaelezwa huduma ya maji inapatikana kwa asilimia 73.2 kwa mwaka 2020 kiasi ambacho kimepanda kutoka asilimia 61.6,2015 huku vijijini ikipatikana kwa asilimia 73.2 na mijini 73.3.
Akiweka bayana jitihada zinazochukuliwa na serikali katika kuboresha sekta ya maji ,wakati wa ziara ya kikazi mkaoni Njombe katibu mkuu wa wizara ya maji mhandisi Antony Sanga amesema huduma ya maji ni muhimu kwa binadamu hivyo tayari wakandarasi wameanza kuchukua hatua za awali za utekelezaji wa miradi hiyo hatua ambayo imemfanya mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya kushindwa kuzuia hisia zake.
Mbali na miradi hiyo katibu mkuu ametembelea na kukagua mradi wa Ilolo-Bulongwa ambao umeanza kujengwa kwa nguvu za wananchi na kisha kuweka bayana kwamba rais ameona jitihada za wakaZi hao kupitia video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kutoa mil 100 za awali kuwaunga mkono.
Nao wananchi akiwemo Edson Swalo,Jane Mwakagile pamoja na mbunge wa Makete Festo Sanga wanasema kwa muda mrefu wamekuwa wahanga wa huduma ya maji na kudai kwamba kuna kilasababu ya serikali kutekeleza mradi huo uliosanifiwa miaka miwili iliyopita.