Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato (pili kulia) akipita kukagua Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme wa Kilovolts 400 cha Lemuguru kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo, Februari 17, 2021.
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato (kulia) akitoa maelekezo kwa wasimamizi na watekelezaji wa ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme wa Kilovolts 400 cha Lemuguru kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo, Februari 17, 2021.
Baadhi ya nguzo zitakazobeba mitambo katika Kituo cha Kupoza Umeme wa Kilovolts 400 cha Lemuguru kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato alifanya ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho mkoani humo, Februari 17, 2021.
Wafanyakazi katika Kituo cha Kupoza Umeme wa Kilovolts 400 cha Lemuguru kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakimueleza jambo Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Februari 17, 2021.
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato (pili kulia) akipita kuona hatua ya ujenzi wa jengo la maalum la kuendeshea mitambo (Control Room) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme wa Kilovolts 400 cha Lemuguru kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, Februari 17, 2021.
Ujenzi wa nguzo zitakazobeba mitambo katika Kituo cha Kupoza Umeme wa Kilovolts 400 cha Lemuguru kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Februari 17, 2021.
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, akikagua nguzo iliyokamilika kujengwa katika Kituo cha Kupoza Umeme wa Kilovolts 400 cha Lemuguru kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo, Februari 17, 2021.
Ujenzi wa jengo maalum la kuendesha mitambo ukiendelea, katika Kituo cha Kupoza Umeme wa Kilovolts 400 cha Lemuguru kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Februari 17, 2021.
……………………………………………………………………………………
Na Zuena Msuya Arusha,
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amekagua ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme wa 400kV cha Lemuguru kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha na kusema kuwa kasi ya ujenzi huo hairidhishi.
Byabato alisema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua kituo hicho iliyofanyika Februari 17, 2021 katika Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha akiwa njiani kuelekea mkoani Manyara.
Alisema kuwa kituo hicho kinatakiwa kukamilika mwezi wa Machi mwaka huu 2021, lakini baada ya kukagua na kuona hali halisi ya kasi ya Ujenzi inavyoendelea, haridhishwi na utekelezaji wa mradi huo.
Kufuatia hali hilo aliwataka wakandarasi wanaotekeleza Ujenzi huo pamoja na wasimamizi kufanya kazi usiku na mchana ili ili kuhakikisha kazi hiyo inakwenda haraka na kukamilika kwa wakati uliopngwa.
Hata hivyo Byabato alisisitiza kuwa, licha ya kuagiza kufanya kazi usiku na mchana, watekelezahi hao wafanya kazi kwa kasi, ubunifu na kwa usahihi kama kauli mbiu ya wizara inavyioelekeza na kusiepo kwa visingizio.
“Siridhiswi na kasi ya ujenzi unaoendelea hapa, kituo hiki kinatakiwa kumalizika haraka, wanachi wanataka umeme, kumbukeni kuna vijiji 19 vinategemea kupata umeme baada ya Kituo hiki kukamilika, ongezeni nguvu kazi, mfanye kazi usiku na mchana, na muifanye kwa usahihi, kasi na kwa ubunifu mkubwa”, alisema Byabato.
Katika hatua nyingine alilitaka Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuharakisha kujenga barabara inayopita katika eneo la kituo hicho kwenda katika Kijiji jirani yenye urefu wa zaidi ya kilometa tatu (3), kwa kiwango cha changarawe kwa gharama nafuu kwa kuwa changarawe hiyo inapatikana maeneo hayo.
Aidha aliitaka TANESCO kushirikiana na uongozi wa kijiji hicho ili na wao wawe sehemu ya mradi huo, waone manufaa yake na kuharakisha ujenzi huo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi alimuomba Naibu Waziri hiyo kufuatilia malipo ya fidia kwa wananchi wachache waliobaki kulipwa baada kupisha mradi huo.
Aidha ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Nishati kuendelea na kazi ya kusambaza Umeme katika vijijini mbalimbali nchini, na tayari mpango wa kuvifikia vitongoji vyote unaendelea.
Kituo cha kupoza umeme cha
Lemuguru, kitatumika pia kusafirisha umeme 400kV hadi katika eneo la
Isinya nchini Kenya, kitakuwa na uwezo wa kupoza umeme wa 222kV, na 35kV
kwa ajili matumizi mengine.