NAIBU WAZIRI WA MAJI ATENGUA NAFASI ZA MAMENEJA MAJI SONGWE

 


NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Marryprisca Mahundi ametengua nafasi za mameneja wawili wa Mamlaka za maji mkoani Songwe kwa kushindwa kusimamia miradi mbalimbali ya maji katika Wilaya zao.

Waliotenguliwa ni Kaimu Meneja wa Maji katika Mji wa Tunduma, Peter Clement ambaye licha ya Serikali kutoa kiasi cha fedha shilingi Bilioni tatu nukta tatu lakini ameshindwa kuusimamia pamoja na Meneja  wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vwawa na Mlowo, Akiba Kibona kwa kushindwa kutimiza majukumu yake inavyotakiwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post