Grace Gurisha
NAIBU Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema jukumu la Wizara hiyo ni kuibua vipaji na wakishaviibua ni lazima wavilee, wavikuze ili kufikia sehemu ambapo vinaweza kutoa huduma au bidhaa ambayo inaitaka kwenye jamii.
Kipanga amesema hayo leo Januari 6,2021 alipotembelea Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania (COSTECH) ikiwa ni moja ya ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza, kukutana na wafanyakazi na kama kuna changamoto wazifanyie kazi.
Amesema katika kujifunza ameweza kutembelea maeneo mawili la kwanza wabunifu ambao wabuni kitu fulani au jambo fulani, ambapo wanawekwa sehemu moja ili mawazo yao kuweza kulepeleka kwenye vitendo, lengo ni kukuza kile kipaji chake alicho kibuni
"Eneo la pili tumekwenda kwenye lile wazo ambalo limeshakuwa, nakuona namna gani ya kuweza kumlea kwa kutengeneza kampuni, lakini pia wazo lake alilokuwa nalo kwenda kuliuza kwenye utoaji wa huduma," amesema Kipanga
Naibu huyo amesema, kazi inayofanyika ni kubwa, inatakiwa ienzie na isimamiwe vizuri ili kuhakikisha wanatoka hapo walipo na kupiga hatua mbili mbele zaidi ,ambapo kama kuna changamoto watazifanyia kazi ili Serikali tuwe na kauli moja ya kitu ambacho tunafanya.
Akizungumza Sera ambazo wabunifu w alitaka ziwe nafuu, Kipanga amesema walichokuwa wanazungumza kuwa wakisha lelewa wanapokwenda kuanza kuzalisha, zile kampuni zinapoanza kufanya kazi, hakuna muda wa wao kuwalea ili waweze kukuwa.
"Ile siku ya kwanza tu kampuni inaposajiliwa mamlaka zingine za kisheria, mfano TRA zinakwenda katika uwanja wa sheria kuwa unatakiwa ulipe tozo hizi au ulipe stahiki zinazohitakika kisheria, hapa ndipo tunapoona kuna changamoto kwa hiyo ni eneo ambalo linahitaji muunganiko,"
"Kumbe sisi kama Wizara tukishamaliza kuwalea kampuni zinapoanzishwa labda kuwe kuna muda, unapokopa kwenye benki huwezi kukopa leo, kesho ukaanza kurudisha kwa sababu unaenda kufanya uwekezaji lazima kupata muda wa kuwalea na kuwakuza kabla ya kuanza kuwatonza kodi na tozo," amesema
Kipanga amesema suala hilo, wamejadiliana na menejimenti kuwa wakae na wenzao wa viwanda na biashara, Wizara ya fedha, Wizara ya Mipango, Wizara ya kilimo ili kuweza kuwakuza waje kuwasaidia watanzania wengi.
"Rais Dkt. John Magufuli alisema tunahitaji mabilionea wengi katika kipindi cha miaka mitano, kumbe mabilionea tunaweza kuwapata kwa kuwazalisha hapa time kwa kutumia Teknolojia yetu ya ndani," amesema
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu amesema ile ndoto ya Rais Dkt. Magufuli ya uchumi wa viwanda , tume hiyo ni sehemu ya kuisaidia Wizara hiyo, kwenda kwenye uchumi huo kupitia wabunifu na watafiti ambao kwa badae wataanzisha viwanda hapa nchini.
Amesema rais anajitaidi kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia kwenye uchuni wa kati wa juu, kama alivyozungumza wakati alipofungua Bunge na kutangaza baraza la mawaziri, ambapo alianzisha Wizara mpya inayohusika na Habari na Teknolojia, kwa hiyo tume haitamuangusha kufikia maendeleo hayo.
"Mchango wa tume ni kuhakikisha tafiti na ubunifu zote zinafanya kazi pamoja kwa lengo moja , kama Naibu Waziri alivyosema tunawakusanya pamoja na kuwajenga, kuwalea kwa lengo la kuwakuza zaidi," amesema Dkt. Nundu
Amesema wataendelea kuishauri Serikali kuwa iisiishie kuwalea tu na pia wawaandalie mazingira wezeshi ya wao kwenda mbele zaidi.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzungumza na Menejimenti ya COSTECH jinsi watakavyoshirikiana kuwalea na kuwakuza wabunifu wa vitu mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari kuhisiana na mipango ya kuwafanikisha wabunifu na watafiki kufika mbali zaidi.