NAIBU WAZIRI OMARI KIPANGA AKIPONGEZA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

 



Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amekipongeza Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kutimiza malengo  na kuwa na mafanikio katika maeneo mbalimbali Chini ya Uongozi na Utawala wa Mhe. Rais John Pombe Magufuli.


Naibu Waziri  Kipanga ameyasema alipofanya ziara ya kikazi ambayo imelenga kujifunza namna Chuo kinavyojiendesha lakini pia kubaini changamoto ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi.


Akitoa tathmini ya mafanikio ya Chuo hicho Mkuu wa Chuo Prof. Shadrack Mwakalila amesema ndani ya miaka mitano ya Utawala wa Mhe. Rais John Magufuli Chuo kimekuwa na mafanikio mengi, baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na Kuongezeka kwa  idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa chuoni hapo kutoka wanafunzi 1592 hadi 11, 413, kuongezeka kwa  idadi ya wahitimu kutoka 569 mwaka 2015 hadi kufika 4696 kwa sasa na kuongezeka kwa idadi ya Wafanyakazi 168 mwaka 2015 hadi  285 kwa wanataaluma na Waendeshaji.


Prof.Mwakalila pia amebainisha kuongezeka kwa programu zinazotolewa Chuoni hapo kutoka programu 3 kwa mwaka 2015 hadi kufikia programu  10 kwa sasa, Chuo kimeboresha mitaala kwa kuingiza mitaala mipya ya uongozi, maadili na Utawala bora  na pia Chuo kimeboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa kufunga Viti visivyohanishika.


Naibu Waziri Kipanga ametumia ziara hiyo kukagua miundombinu mbalimbali ya Chuo ikiwemo Maktaba ya Chuo, Idara ya TEHAMA, jengo la ukumbi wa mihadahara lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 kwa mara moja na kukagua ukuta uliojengwa pembezoni mwa bahari kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi.


IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA HABARI NA MAHUSIANO

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

08.01.2021

Post a Comment

Previous Post Next Post