WAZIRI WA KILIMO PROF. MKENDA AIPONGEZA TARI KWA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU KUHUSU UZALISHAJI WA MICHE YA MICHIKICHI

 Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akifuatilia wasilisho kuhusu maendeleo ya uzalishaji wa mbegu pamoja na miche bora ya zao la chikichi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) wakati alipotembelea Kituo mahiri cha Utafiti wa zao la chikichi (TARI Kihinga kilichopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji leo tarehe 18 Desemba, 2020. Waziri Mkenda yupo mkoani Kigoma kwenye ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

 

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akipata maelezo kutoka Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) wakati alipotembelea Kituo mahiri cha Utafiti wa zao la chikichi (TARI Kihinga) kilichopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, leo tarehe 18 Desemba, 2020.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akiagana wa Watumishi wa Kituo cha TARI Kihinga wakati alipotembelea Kituo hicho kilichopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, leo tarehe 18 Desemba, 2020. Waziri Mkenda yupo mkoani Kigoma kwenye ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya wakimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma ili kuanza ziara ya siku mbili ambapo anataraji kutembelea Kituo cha TARI Kihinga pamoja na kuzungumza na Wadau wa zao la chikichi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kesho tarehe 19 Disemba, 2020.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia burudani ya ngoma kutoka kwa kikundi cha ngoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mkoani Kigoma leo tarehe 18 Desemba, 2020 ili kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo.

Post a Comment

Previous Post Next Post