WAFANYA BIASHARA WATAKIWA KULIPA KODI


 KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede katikati mstari wa chini akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa na baadhi ya wafanyabiashara mkoa wa Iringa.

………………………………………………………………………….
NA DENIS MLOWE,IRINGA
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede ametoa rai kwa wafanyabiashara nchini kuwa wazalendo kwa kuendelea kuwa walipa kodi kwa wakati kama sehemu ya kuchangia mchakato wa ujenzi wa Taifa.
Akiongea wakati wa mkutano wa wadau wa maendeleo na wafanyabiashara mkoani Iringa, Dk.Mhede alisema suala la ulipaji wa kodi ni ishara ya uzalendo na linapaswa kufanywa bila ya kusukumwa kwani ni jambo ambalo lina mchango chanya ktk ujenzi wa nchini.
  
Alisema kuwa ulipaji wa Kodi ni tendo takatifu kwa nchi yoyote hivyo ni jukumu la kila mmoja kuweza kulipa Kodi kwa wakati ili kuwezesha serikali kuharakisha maendeleo ya nchi.
Alisema kuwa moja ya mikoa iliyofanya vyema katika ulipaji wa Kodi ni mkoa wa Iringa na kuipongeza serikali ya mkoa na Mamlaka ya TRA kwa kazi nzuri na kuwataka kuendelea kuwa walipa Kodi wazuri nchini 
Dk. Mhede alisema kila mkoa uliwekea malengo ya ulipaji Kodi ambapo mkoa wa Iringa ulifikisha asilimia zaidi ya 95 kwa mwaka wa Kodi uliopita akiongeza kuwa mwaka huu wameongezewa kiwango cha Kodi waweze kufikia malengo.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi wa mkutano huo wa siku moja, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi alisema wakati umefika sasa kwa wizara inayohusu masuala ya elimu kuliingiza somo la ulipaji wa kodi ktk mtaala ili elimu inayotolewa kwa watoto iendane na umuhimu huo wa kodi.

Post a Comment

Previous Post Next Post