Na MwandishiWetu Dodoma
Mkurugenzi Rasimali watu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi. Mary Mwangisa, amewapa maekelezo baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo watakaoshiriki katika zoezi la utoaji elimu na mafunzo ya utunzaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliji katika baadhi ya skimu za kilimo hicho nchini.
Akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Bi Mwangisa amesema kuwa watumishi hao wanapaswa kuzingatia mwongozo wa namna ya kutoa mafunzo ya vyama vya umwagiliaji wa namna ya kukusanya mapato kwa ajili ya uchangiaji wa mfuko wa maendeleo ya umwagiliaji, matumizi sahihi ya kalenda za kilimo na utunzaji wa miundombinu ya umwagiaji.
“Serikali imewekeza pesa nyingi katika miundombinu ya umwagiliaji kwa hiyo isipotunzwa serikali itapata hasara, na wakulima wataathirika, vyama vya umwagiliaji vitakufa na miundombinu hiyo itakufa.” Alisisitiza.
Aliendelea kusema kuwa kilimo cha umwagiliaji ni moja kati ya mategemeo ya kuongeza uzalishajiwa mazao ya chakula na biashara na uhakika wa usalama wa chakula nchini.
Maelekezo hayo kwa watumishi yametolewa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkakati wa tume ya taifa ya umwagiliajiwa kutoa elimu kwa vyama vya umwagiliaji nchini.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi Mary Mwangisa, akitoa maelekezo wa baadhi ya watalaam watakaoshiriki katika elimu ya mafunzo na matunzo ya miondombinu ya umwagiliaji kwa wakulima.Mkurugenzi msaidizi wa idara ya mafunzo na matunzo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Enterbert Nyoni akifafanua jambo wakati wa kikao na wataalam,cha maandalizi ya utoaji elimu kwa wakulima kuhusiana na utunzaji wa miundominu ya Umwagiliaji.kulia, ni Bw.Reginald Diamett Meneja Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji.Picha ikionesha sehemu ya washiriki katika kikao hicho cha maandalizi.