WADAU WA NYAMA WENYE MABUCHA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA VIFAA VYA KISASA VYA KWENYE MABUCHA

 

Kaimu Msajili Bodi ya Nyama Tanzania huyo aliyevaa (koti la suti) Imani Sichalwe akiwa na viongozi wa wadau wa Nyama Arusha,viongozi wa kampuni ya watertras na viongozi wa Amana benki. 
Kaimu Msajili Bodi ya Nyama Tanzania huyo aliyevaa (koti la suti) Imani Sichalwe akikagua moja ya mashine za kisasa za kukatia nyama vitakavyosambazwa na Kampuni ya watertras

 
 =======   =====   ======   =====
 
 
 Na.Vero Ignatus.


Wadau wa Nyama Nchini watakiwa kujiunga Kwenye vikundi na visajiliwe kwa mujibu wa sheria ,Jambo litakalowawezesha kuwa na Vigezo vya kukopesheka kwenye Taasisi mbali mbali za kifedha Nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Nchini Tanzania Imani Sichalwe ,mara baada ya kumalizika kikao kazi kilichofanyika mkoani Arusha kikihusisha viongozi wa Amana bank, viongozi wa wauzaji nyama Arusha, viongozi wa kampuni ya watertrans  Lengo likiwa ni kujadili na kukubaliana kwa pamoja ni namna gani wauzaji nyama Kwenye mabucha wanaweza kukopesheka.

 Sichalwe amesema ni muda mrefu wadau wa nyama ,wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kutokukopesheka kutokana na masharti yaliyopo kwenye baadhi ya Taasisi za kifedha, kuwa na masharti mbalimbali ambayo wengi wao hushindwa kuyatimiza na kujikuta wanakosa sifa za kukopesheka

 Amewapongeza benki ya Amana pamoja na kampuni ya watertrans, ambao ndio wasambazaji wa vifaa hivyo vya kisasa vya kuchakata nyama kwenye bucha, kwa  kuona umuhimu wa kukopesha wadau wa nyama wenye mabucha kwa masharti nafuu jambo ambalo litaongeza tija kwenye Tasnia ya Nyama Nchini.

Amefafanua  kuwa wafanyabiashara ya nyama kwenye bucha, wanachotakiwa ni kujiunga kwenye vikundi vya wauza nyama vilivyosajiliwa, ambapo ndio kigezo kikubwa cha kuwa na sifa ya kukopesheka, na kutakiwa kurejesha mkopo huo kwa muda wa mwaka mmoja.

Aidha Kaimu Msajili huyo wa Bodi ya Nyama Tanzania Imani Sichalwe ,amewataka  Maafisa biashara wa halmashauri na Maafisa mifugo kuhamasisha wadau wa nyama ,wajiunge kwenye vikundi vilivyosajiliwa ili waweze kukopeshwa vifaa vya kisasa vya kwenye bucha.

Mpango  wa ugawaji wa vifaa hivyo vya kisasa kwenye bucha kwa awamu ya kwanza ,unatarajiwa kufanyika tarehe 4 November 2020 Mkoani Arusha, na wadau wa nyama wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo ,kwa kujisajili kwenye vikundi vya wadau wa nyama vilivyosajiliwa ili kuwa na sifa ya kukopesheka

"Lakini pia ni ukweli usiopingika kuwa Sasa hivi tunashuhudia mabadiliko makubwa za kiteknolojia za vifaa Kwenye bucha kutokana na watu wengi kuondokana na matumizi ya gogo la kukatia nyama,matumizi ya mizani ya kizamani na n.k kwa hivyo mpango huu utasaidia kuboresha Miundombinu ya Kwenye bucha zetu na kuwa za kisasa."

Sichale ameongeza kwa kusema kuwa mpango wa ukopeshaji wa vifaa vya kisasa kwenye bucha utasaidia kwa kiasi kikubwa  kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Bodi ya Nyama Tanzania inayosema "Nyama Bora na Salama kwa wote" 

Aidha mikopo hiyo ya vifaa vya kisasa vya Kwenye bucha inatolewa na Amana benki ,kwa ushirikiano wa kampuni ya watertrans ,ambao ndio wasambazaji wa vifaa hivyo vya kwenye bucha,ukiratibiwa na Bodi ya Nyama Tanzania na kwa kuanzia utaanzia mkoani Arusha kisha utatekelezeka nchi nzima

Post a Comment

Previous Post Next Post