DAWASA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WADAIWA SUGU

  Na Karama Kenyunko Michuzi TV


WADAIWA sugu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), wa maeneo ya Tabata, Ubungo, na Buguruni Mnyamani wamefikishwa katika Mahakama  ya Mwanzo Ilala kizimbani  maji wa maeneo ya Tabata, Ubungo, na Buguruni Mnyamani katika Makidaiwa bili za maji ya jumla ya Sh. 8,015,187.4.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Afisa sheria kutoka DAWASA, Omary Kipingu imewataja washtakiwa waliofika leo kuwa ni, Ahad Gurisha Mkazi wa Kisukuru, Tabata anadaiwa 2,957,162, ambapo amepunguza Sh.400,000, Tune Juma Mkazi wa Kibangu, Ubungo anadaiwa 584,707.15,

Washtakiwa wengine ambao hawajafika leo licha ya mahakama kutoa hati ya wito wa kuitwa mahakamani ni, David Mgaya (Tabata) ambae anadaiwa Sh. 1,085,178.15,  Rahima Sarakikya Mkazi wa Buguruni anadaiwa 747,852.45, Hassan Khamis Mkazi wa Buguruni Mnyamani anadaiwa Sh.733,008.45, Zacharia Okoth Mkazi wa Tabata anadaiwa Sh.592,964.35 na Ashura Embe Mkazi wa Buguruni Mnyamani ambae anadaiwa Sh.1,314,314.85.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mbele ya mahakimu wawili tofauti ambapo, Gurisha na Juma wamesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Nahato na kwamb walikubali kuwa ni kweli wanadaiwa na mamlaka hiyo.

Gurisha na Juma ,baada ya kusomewa makosa yao na Ofisa  wa Sheria kutoka Dawasa, Omary Kipingu mbele ya Hakimu Mkazi, Nahato wa Mahakama hiyo walikubali kuwa ni kweli wanadaiwa na mamlaka hiyo.

Hivyo, walikubali kuingia mkataba wa makubaliano wa kulipa deni hilo hadi liishe, ambapo Gurisha amekubali kulipa 320,000 kila tarehe 28 ya mwezi kwa miezi sita, aliahidi kumaliza deni hilo Aprili 28, 2021.

Kwa upande wake, Juma aliyeingia makubaliano ya kulipa dei hilo ni mama mwenye nyumba wake, Gregory Kahwili ambae aliahidi kuwa Septemba 30,2020 atalipa 200,000, ambapo deni lililobaki atalipa kila mwezi 100,000 litakamilika Januari 30,2021.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imetoa agizo la mwisho kwa wadaiwa hao kufika mahakamani hapo, ambapo imetoa hati ya wito kwa wadaiwa hao ambao watatakiwa kufika mahakamani  hapo, Septemba 11, mwaka huu. Mwanasheri wa Dawasa, Omary Kipingu katikati akiwa na wafanyakazi wa DAWASA, kulia ni Sofia Owe Afisa huduma wa wateja na kushoto ni Burton Mwalupaso ambaye ni Afisa biashara DAWASA Tabata wakiwa nje ya viung vya mahakama ya Mwanzo Ilala baada ya wadaiwa sugu hawapo pichani kumaliza kusomewa mashtaka yao n kukiri kulipa bili zao.

Post a Comment

Previous Post Next Post