RC NDIKILO AFUNGUA RASMI MADARASA MAWILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MKONGO WILAYANI RUFIJI

 

Mkuu Mkoa wa Pwani wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikata utepe kuashiria zfunguzi rasmi wa madarasa mawili katika shule ya sekondari Mkongo,kushoto kwake ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Patriki Salawa ikiwa ni ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kugagua shughuli mbali mbali za kimaendeleo.

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katikati akiwa na viongozi wengine wa serikali kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Patrick Salawa.

Baadhi ya wanafunzi wa wanaosoma katika shule ya sekondari Mkongo iliyopo Wilayani Rufiji wakiwa shuleni hapo wakipiga kwata ikiwa ni ishara ya heshima ya kumpokea Mkuu wa Mkoa wa Pwani aliyefika shuleni hapo kwa ajili ya kuzinduzua madarasa mawili.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ameketi kwenye dawati katika mojaya chumba cha darasa ambalo amelizindua katika shule hiyo ya sekondari ya Mkongo alipokwenda kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere aliyeketi kulia akiwa anatabasamu kwa furaha uku akiwa ameketi kwenye dawati lililopo katika moja na darasa jipya ambalo limezinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist ndikilo wa kati kati akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mkongo wakati walipofanya ziara yake ya kikazi pamoja na kuzindua madarasa mawili katika shule hiyo.(PICHA  ZOTE NA VICTOR MASANGU)

……………………………………………………………..

NA VICTOR MASANGU, RUFIJI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo Evarist Ndikilo amewataka wazazi na walezi kuachana kabisa  na tabia ya kuwakatisha masomo watoto wao kwa sababu zisizo za msingi na badala yake wahakikishe wanaunga juhudi za Rais wa awamu ya tano  ya Dk. John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu.

Ndikilo ametoa kauli wakazi wa halfa fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya  uzinduzi rasmi wa   madarasa mawili katikashule ya sekondari Mloka ikiwa ni mwendelezo  wa  ziara  yake ya kikazi yenye lengo la kutembelea  miradi  mbali mbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili  wananchi.

“Kwa kweli wazazi na walezi mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani ninawaomba sana wazazi na walezi hii tabia ya kuwakatisha masomo watoto wenu sijaipenda inatakiwa mbadilike na kuhakikisha kwamba mnawapatia haki zote amabzo wanastahili katika suala zimala uapatikanaji wa elimu kwa hivyo katika Mkoa wa Pwani sitaki kuliona suala hili,”alisema Ndikilo.

Aidha alisema kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha sekya ta elimu katika shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika suala zima la elimu bila ya kuwepo kwa ubaguzi wowote.

Aidha Ndikilo alibainisha kwamba pia serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya majengo ya shule kongwe za sekondari pamoja na kuyafanyia ukarabati majengo ambayo yamechakaa ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki na kuziagia halmashauri zote kuweka mipango madhubuti ya kutengeneza madawati na meza ili kuondokana na adha ya kusoma kwa mlundikano.

Kwa uapnde wake Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Patriki Salawa aliahidi kutekeleza maagizo yote ambay yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kwamba atahakikisha anapmbambana vilivyo kuona wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri na kwamba ataendelea kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo.

“Mkuu wa Mkoa mimi nimepokea maelekezo yako na kiukweli pamoja yote nimshukuru sana Rais wa awamu ya tano Dk, John Pombe Magufuli kwa kuwez akuniteuwa katika nafasi hii ya Mkuu wa Wilaya ya Rufiji nitafanya kazi kwa weledi kwa kushirikiana na viongozi wenzangu ili kuweza kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa ujumla.”alisema Salawa.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Pwani ameamua kulivunja baraza la ardhi la kata ya ikwiriri kusini kutokana na kulalamikiwa na wananchi kwamba halitendi haki katika maazuzi yake pindi linapotaka kusuluhusiha kesi za migogoro ya ardhi pamoja na masuala ya migogoro ya wakulima na wafugaji.

“kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi amabyo yanatolewa na wananchi kuhusiana na kuwepo kwa mapungufu mnakubwa katika baraza la ardhi la kata ya ikwiriri kusini kuanzia leo ninalivunja baraza hili na ninaelekeza kwamba ufanyike utaratibu mwingine wa kuwachagua  viongozi wengine ambao wana nian ya kutatua migogoro ya  ardhi.

Kadhalika Mkuu huyo wa Mkoa  wa alisema kwamba amebaini  baadhi ya watendaji wa vijiji na vitongozi baadhi yao ndio wanahusika kuuza maeneo kiholela bila ya kuzingatia  sheria na taratibu zilizowekwa nndio maana kunasababisha kuwepo kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hivyo amewataka kuchapa kazi kwa weledi.

“Hii migogoro amabyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara  nimegundua inachangia na baadhi ya watendaji wetu wa vijiji pamoja na vitongozi hivyo ninatoa muda wa mwezi mmoja endapo kama kuna eneo lolote kama nikine kunaendelea na vurugu hizi basi mtendaji mwenyewe ajue hana kazi kabisa na ili nimeamua kuliweka wazi na nitawachukulia hatua kali zaidi,”alisema Ndikilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post