AFISA wa
Brela Nassoro Shomari Mtavu kulia
akikabidhi cheti cha jina la Biashara kwa mtumiaji huduma za Wakala baada
ya kukamilisha taratibu za usajiliAfisa kutoka Brela
Bi Sada Kilabula kushoto akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda lao
kwenye maonyesho ya nane nane mkoani Lindi
Brela Nassoro Shomari Mtavu kulia
akikabidhi cheti cha jina la Biashara kwa mtumiaji huduma za Wakala baada
ya kukamilisha taratibu za usajiliAfisa kutoka Brela
Bi Sada Kilabula kushoto akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda lao
kwenye maonyesho ya nane nane mkoani Lindi
Team
ya Brela ikiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Bakari Ally Mketo
wa pili kutoka kushoto wakiwa tayari katika banda Banda kutoa huduma
Afisa kutoka Brela Bi Sada Kilabula kulia akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda lao kwenye maonyesho ya nane nane mkoani Lindi
WAKALA wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeshiriki maonyesho ya wakulima nane nane kwenye mikoa ya Simiyu na Lindi ili kuweza kuwafikia zaidi wananchi wake katika utoaji wa elimu ya kurasimisha biashara na huduma zinazotolewa na wakala huo.
BRELA ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo jukumu la taasisi ni kusajili majina ya Biashara, makampuni, nembo za huduma na biashara, Hataza, Utoaji wa leseni za Biashara daraja A na Leseni za Viwanda.
Katika Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho hayo wakala huo uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Utawala na fedha Bakari Mketo ambaye alibainisha kwamba lengo kuu la kushiriki katika maonesho hayo ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma na utatuzi wa changamoto wanazokutana nazo wakati wa kufanya sajili mbalimbali za BRELA papo kwa papo.
Pamoja na yote amewataka wakulima na wadau mbalimbali kuweza kurasimisha biashara zao ili kutambulika na kuweza kuufikia Uchumi wa kati.
Pia ameeleza kwamba dhumuni la kushiriki maonesho ni kuwasogezea wananchi wa lindi huduma kwa ukaribu na kuendelea kutoa mafunzo juu ya utumiaji wa mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatembelea katika banda lao lililopo katika viwanja vya Ngongo ili kuweza kupata huduma za sajili papo kwa papo.