Pemba, Msumbiji.

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amepokea Uenyekiti wa Kamisheni ya Bonde la Mto Ruvuma, Uenyekiti huo utadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo Serikali ya Jamhuri ya Malawi itakuwa Makamu Mwenyekiti. Pemba, Msumbiji.

Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Msumbiji na Malawi kupitia Viongozi wa Sekta yapo Maji katika nchi hizo leo tarehe 31 Julai, 2026 zimesaini Mkataba wa kuanzisha Kamisheni ya Bonde la Mto Ruvuma. 

Tukio hili la Kihistoria limehusisha utiaji saini kwa wawakilishi wa nchi ambapo ikiwa ni pamoja na Mhe. Jumaa Aweso Waziri wa Maji wa Tanzania pamoja na Mawaziri wa Maji wa Msumbiji na Malawi kwa uwakilishi wa Makatibu Wakuu wa Sekta ya Maji.

Washiriki wengine katika Hafla hiyo ni Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe Khamis Hamad, Balozi Mdogo wa Serikali ya Ujerumani nchini Msumbiji, Gavana wa Jimbo la Pemba Msumbiji, pamoja na Wadau wa Maendeleo (IUCN, GWPSA, GIZ, na WI). 

Mkataba huu utaongeza chachu ya usimamizi wa rasilimali za maji kwa njia shirikishi baina ya nchi wanachama na wadau wote walipo katika Bonde la Mto Ruvuma ambapo Serikali ya Tanzania itanufaika kwa kuwa Mto Ruvuma ni moja ya vyanzo vitakavyotumika katika Grid ya Taifa ya Maji.