CHONGOLO: SOGEZENI MBOLEA KWA WAKULIMA


  Mwandishi Wetu,                                            Serikali imeagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha inasema usambazaji wa mbolea kwa wakulima nchini wakiwemo wakulima wa kijij cha Mang’ola, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Amesema Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo, ili kukagua miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Bw. Samwel Mshote amesema kuwa tani elfu mbili za mbolea ya DAP zinapelekwa ndani ya wiki mbili katika kijiji hicho huku taratibu za kuwa na Mtendaji Mkuu wa TFC kuwepo Mang’oa zitatekelezwa ili wakulima wapatiwe elimu ya matumizi sahihi ya mbolea.

Sambamba na hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Joel Laurent ,amesema kuwa wakulima wataendelea kupatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea kupitia Kampeni ya Mali Shambani inayoratibiwa na Wizara ya Kilimo kuanzia mwezi Agosti 2026 .

Ameeleza kuwa “matumizi mbadala si kununua mbolea kwa jina badala yake ni kuwa na elimu ya sahihi ya matumizi ya molea kwa kuendana na virutubisho, afya ya udongo na mbegu bora.”

Kuhusu biashara holela ya mbolea, Bw. Laurent amesema kuwa hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza mbolea kinyume na masharti ya leseni yake na moja ya adhabu ni kufutiwa leseni. 

Mpango wa ruzuku bado upo kupitia maelekezo ya Serikali ambayo imetoa fedha kuhakikisha mkulima anapata bei himilivu ya mbolea.

Post a Comment

Previous Post Next Post