
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Wizara ya Maliasili na Utalii imefumbua rasmi fumbo la #ATM2030 kwa kuonesha safari ya kuelekea watalii milioni 8 ifikapo mwaka 2030 inavyoendelea.
Akifumbua fumbo hilo jijini Arusha leo Aprili 19, 2026, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameitambulisha ATM 2030 ikimaanisha AT (Eight) yaani 8, M ikimaanisha idadi ya watalii milioni 8 na 2030 ikimaanisha mwaka wa kikomo wa kufikisha idadi hiyo ya Watalii Milioni 8 ifikapo 2030 kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Katika kufumbua fumbo hilo kwa kuonesha idadi ya watalii waliofikiwa mpaka sasa, imeelezwa kuwa kwa mwaka 2025 idadi ya watalii inchini imevunja rekodi ya malengo ya awali ya Ilani iliyorlekeza kufikiwa watalii milioni 5, ambapo kwa idadi mpya iliyotangazwa leo watalii wamevunja rekodi kwa kufikia milioni 5.9.
“Tumevunja rekodi ya Ilani ya awali ya milioni 5 na kwa takwimu hizi sasa maana yake ni kwamba safari ya kuelekea nilioni 8 za lengo jipya la Ilani inaanza vyema tukiwa tumevunja rekodi ya Ilani iliyoisha,” alisema.
