MAWAKILI 30 WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI WAHITIMU MAFUNZO YA PPP CERTIFICATION

 

Mawakili 30 kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamehitimu Mafunzo ya kitaalamu yanayohusu Masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Certification Course).

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku Saba Mkoani Arusha katika Ukumbi wa Hotel ya Lush Garden kuanzia tarehe 9 hadi 15 Aprili, 2026, ambapo Mgeni Rasmi wakati wa kufunga Mafunzo hayo alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) Bw. David Kafulila.

Aidha, kwa kuzingatia moja ya nguzo ya Dira 2050 ni kuwa na Uchumi imara, Jumuishi na Shindani unaotegemea Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kuhamasisha Uwekezaji, Ubunifu na rasilimali kutoka Sekta Binafsi katika kutekeleza Miradi mikubwa na ya Kimkakati.

Hivyo, kukamilika kwa mafunzo haya kutawajengea uwezo Mawakili wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika masuala ya Upekuzi wa Mikataba ya kimkakati ya Ubia, Majadiliano (Negotiation), Ushauri wa Kisheria kuhusiana na masuala ya ubia na kuandaa Miswada ya Marekebisho ya Sheria yatakayoleta tija katika kufikia uchumi imara na jumuishi, kuimarisha miundombinu na mazingira ya uwekezaji nchini.

Aidha, kwa kuhitimisha mafunzo hayo Tanzania itapanda hadhi kutoka nafasi ya tisa mpaka nafasi za juu duniani kwa kuwa na wataalamu wabobezi katika masuala ya Ubia. 

Katika mafunzo hayo, Mawakili wamejifunza masuala mbalimbali kuhusu Usimamizi wa miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, mchakato wa Manunuzi, pamoja na Uandaaji wa Mikataba ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.

Awamu hii ni hitimisho la mfululizo wa Hatua Tatu ya Mafunzo haya ya Kitaalamu ( PPP Certification) kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hatua ya kwanza ( PPP Foundation Stage) ilifanyika tarehe 3 hadi 6 Februari, 2026 Jijini Dodoma, na Hatua ya Pili ( PPP Preparation Stage ) ilifanyika tarehe 9 hadi 13 Machi, Kibaha Mkoani Pwani

Post a Comment

Previous Post Next Post