PROF. MKENDA AIPONGEZA MKINGA KUTENGA ENEO LA MJI WA WANAZUONI

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda ameupongeza uongozi Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kupitia Mwenyekiti wake Mhe.Amani Juma Kasinga kwa kutenga eneo la kujenga mji wa wanazuoni katika eneo hilo.

 

Akizungumza mara baada ya kukamilisha ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo katika kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe Tanga inayojengwa eneo la Gombera, Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Waziri Mkenda amesema amrfurahishwa na maono ya Halmashauri ya Mkinga kufanya eneo la Gombero kuwa mji wakitaaluma na kuwahamasisha wawekezaji katika sekta ya elimu kuwekeza.“Juzi tumekaa kuzungumzia PPP kwenye elimu ya ufundi, tutahimiza wawekezaji wa eneo la ufundi waje wawekeze hapa, wajenge sekondari za ufundi na kuweka kampasi za vyuo vingine vya elimu kwani ardhi ipo ,”amesema Prof. Mkenda

 

Akizungumzia ujenzi wa kamapasi ya Mzumbe Mhe. Mkenda amesema Kampasi hiyo ni moja ya kampasi zinazojengwa kwa maelekezo ya Mhe. Rais kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi ( HEET) katika mikoa.

 

“Kuna takribani Trilioni moja zimesambaa kwa ajili ya ujenzi wa kampasi za Vyuo Vikuu 15 kupitia Mradi wa HEET,”ameongeza Prof MkendaAmetaja baadhi ya Vyuo vinavyojenga kampasi zake kuwa ni MUHAS Kigoma, UDSM Lindi na Kagera, UDOM Njombe, Chuo Kikuu cha Julius Nyerere Butiama na vingine.

Prof. Mkenda ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kwa kuendelea kusimamia na kuishauri Wizara katika masuala mbalimbali yaliyochangia katika usimamaizi wa uendeshaji elimu kisera na pia kuimarisha utoaji wa elimu bora.

Post a Comment

Previous Post Next Post