REA KUPELEKA UMEME VITONGOJI 474 KAGERA

 

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umemtambulisha mkandarasi wa kutekeleza mradi wa umeme katika vitongoji 474 vya mkoani Kagera kuanzia Februari 2026 hadi Februari 2029.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Yahaya Kido amepokea timu ya wataalamu kutoka REA ambao waliambatana na mkandarasi anayejulikana kwa Jina la CCC International Engineering Nigeria LTD .

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, meneja miradi Kanda ya Ziwa kwa niaba ya Meneja Mkuu, Ernest makale alisema mkoa huo una vijiji 662 na vyote vimpata umeme na mkoa huo una vitongoji 3,665 na kati ya hivyo vitongoji 2029 vimepata umeme.

Alisema vilivyobaki tayari Serikali imeidhinisha vitongoji 474 vinaenda kupata umeme.

Alisema mradi huo utagharimu zaidi ya Sh Bilioni 66.5 na wananchi wa Kagera wapatao 15,396 watanufaika na mradi huo huku mradi wa kusambaza umeme wa vijiji 27 vilivyoko visiwani ukiendelea kukamilika

Alisema mradi huo unatarajia kutoa ajira kwa vijana mbalimbali na kuongeza uzoefu kwa vijana ambao wamesomea maswala ya umeme huku akitaka wananchi kufanya uwekezaji na kujiongozea kipato mara baada ya mradi wa umeme kukamilika

Alisema pia Serikali imefanya mpango wa kuweka transfoma kubwa katika miradi ya umeme Ili wananchi wanaotaka kufanya uwekezaji Vijijini wafanye shughuli za uwekezaji bila changamoto yeyote

Mkuu wa Mkoa Wa Kagera, Kanali Yahaya Kido alitoa wito kwa wakandarasi kutekeleza mradi huo kwa Bidiii na kasi kwa sababu mahitaji ya umeme kwa wananchi hasa vitongojini ni makubwa sana.

Alisema pia wakandarasi wanatakiwa kujitambulisha kwa uongozi wa serikali za vijiji ili kupewa ushirikiano na wenyeviti wa vijiji na wananchi wao katika swala la kulinda miundombinu na kutoa maeneo yao ya kupitsha nguzo za umeme.

Post a Comment

Previous Post Next Post