
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, akizungumza na watumishi wa Wizara wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika Januari 14, 2026, Ukumbi wa wizara Mtumba, Dodoma.
………….
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ameendesha kikao cha pamoja na viongozi wa Menejimenti ya Wizara hiyo kwa lengo la kupitia na kuboresha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Wizara, pamoja na mipango na shughuli zitakazotekelezwa katika mwaka wa fedha 2025/2026.
Katika Kikao hicho kilichofanyika leo Januari 14, 2026 katika Ukumbi wa wizara Mtumba, jijini Dodoma, Dkt. Gwajima amesisitiza umuhimu wa viongozi kusimamia majukumu yao kikamilifu katika utekelezaji wa programu za Wizara katika idara zao ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Viongozi wa Menejimenti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Waziri, Dkt. Dorothy Gwajima, wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika Januari 14, 2026, Ukumbi wa wizara Mtumba, Dodoma.
