SHIRIKA LA UTALII DUNIANI LAPATA BOSI MPYA

Jioni hii Novemba 9, 2025, Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) chombo muhimu katika kutunga sera na kutekeleza mipango ya kuendeleza utalii duniani kwa niaba ya UN, kimeweka historia kwa kumchagua Bi. Shaikha Nasser Al Nowais, raia wa UAE, kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Katibu Mtendaji kuongoza chombo hicho wakati huu sekta ya utalii ikiwa kioo cha mafanikio ya sekta nyingine duniani. 

Shaikha amethibitishwa na Baraza Kuu la UN Tourism kwa kauli moja na wajumbe wote 160 ambapo ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi.

Pichani: Dkt. Abbasi akimpongeza Waziri wa Uchumi na Utalii wa UAE, Mhe. Abdullah Bin Touq Al Marri baada ya upigaji wa kura na ujumbe wa Tanzania ukiwa na Katibu Mtendaji huyo mpya Bi. Sheikha ambaye ameahidi pia kutembelea Tanzania hivi karibuni.



Post a Comment

Previous Post Next Post