Ujenzi wa mabwawa ya takasumu uzingatie sheria na usalama


Mwandishi Wetu,
Serikali inaendelea kuhakikisha ujenzi wa mabwawa ya takasumu unafanyika kwa viwango na kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa  Rasilimali za Maji, pamoja na  usalama.

Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji, Wizara ya Maji Bwn. Heri Chisute amesema katika mkutano wa mwaka unaohusu usalama wa mabwawa.

 Amesema  uhakika wa usalama, utii, na ulinzi wa mazingira si kwa kuangalia sheria pekee bali pia ni wajibu wa maadili kwa jamii zinazotegemea mifumo hiyo kwa ustawi wao ili kuepuka changamoto zinazoweza kutokea kwasababu ya  mabwawa hayo.

Amesema hadi hivi sasa kuna  idadi  ya jumla ya mabwawa ya maji zaidi ya 700 na mabwawa ya taka sumu yakiwa zaidi ya 60.

Mkutano huo  umewakutanisha  watalaamu  mbalimbali kutoka Sekta ya Umma na Binafsi,sambamba na kauli mbiu “Tahadhari za dharura za kukabiliana na Majanga ya mabwawa ya maji na topesumu”
 







Post a Comment

Previous Post Next Post