Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri ametoa maelekezo kwa idara ya Utawala pamoja na maafisa utumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa kufuata miongozo na maadili ya utumishi wa umma.
Mwandisi Mwajuma ametoa maelekezo hayo katika kikao kilichofanyika Oktoba 27,2025 katika ukumbi wa Wizara Mtumba jijini Dodoma.
Pia Mhandisi Mwajuma amesisitiza suala la mabadiliko kwenye maeneo mbalimbali ili kutatua changamoto za kiutumishi kwa watumishi wa wizara hiyo kwa kuzingatia idara na vitengo husika.



