SERIKALI YAPONGEZWA UTEKELEZAJI MPANGO WA RUZUKU YA MBOLEA


 Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepongezwa kwa kuanzisha na kutekeleza mpango wa ruzuku ya mbolea  uliochangia kuongeza matumizi ya mbolea kwa wakulima nchini  na kuchochea uzalishaji wa mazao.

Pongezi hizo zimetolewa  na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaack Anthony, wakati akizungumza na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) iliyopo mkoani Kigoma kwa ziara iliyolenga kuhamasisha upimaji wa afya ya udongo na matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa mkoa huo. 

Kanali Anthony, amesema wananchi wengi wa wilaya yake ni wakulima, na mpango huo wa ruzuku umewasaidia kwa kiasi kikubwa kupata mbolea kwa bei nafuu na kuongeza mavuno.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mjumbe wa Bodi ya TFRA, Khadija Jabri, amewahimiza wakulima na wawekezaji kupima sampuli za udongo kabla ya kutumia shambani ili kuhakikisha wanatumia mbolea sahihi kulingana na mahitaji ya udongo na zao linalolimwa.

Akizungumza mara baada ya kupokea wajumbe hao, mmiliki wa shamba la parachichi, Mhandisi Amon Daniel Ntimba,  ameipongeza serikali kwa kuja na mpango wa ruzuku  ulioleta mapinduzi katika kilimo na kuahidi kuongeza matumizi ya mbolea ili kuzalishaji kwa tija zaidi.

Katika ziara hiyo, wajumbe wa bodi walitembelea  Kiwanda cha Sukari Kasulu na shamba la parachichi la Kibondo Green Farm lililopo wilayani Kibondo.



Post a Comment

Previous Post Next Post