Na Mwandishi wetu, Mwanza
WAFANYABIASHARA mkoani Mwanza wameelimishwa kuhusu mabadiliko mbalimbali ya sheria za kodi ya mwaka wa fedha 2025/26, huku wakihimizwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kulipa kodi kwa wakati.
Akizungumza wakati akifungua semina ya mabadiliko hayo ya sheria iliyofanyika katika ukumbi wa TRA mkoani Mwanza, Meneja wa TRA Mkoani humo Bw. Faustine Mdessa alisema semina hiyo imelenga kuwakumbusha na kuwafahamisha wafanyabiashara kuhusu mabadiliko ya sheria yaliyopitishwa na Bunge ili waweze kulipa kodi stahiki kwa kuzingatia mabadiliko hayo.
“Waelimishaji hakikisheni mnatumia muda wa kutosha ili walipakodi wetu wapate uelewa kwa undani kwa sababu lengo kuu la semina hii ni kuwafahamisha wafanyabiashara mabadiliko haya ili waweze kulipa kodi stahiki kwa wakati”, alisema Meneja Mdessa.
Aidha, Meneja Mdessa aliwasisitiza walipakodi waliohudhuria semina hiyo kumtafuta wakati wowote wanapokutana na changamoto zozote za kikodi ili ziweze kutatuliwa kwa wakati.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka TRA, Bi. Eugenia Mkumbo, alisema mabadiliko ya sheria za kodi yamefanyika ili kupanua wigo wa walipakodi, kuondoa utata wa kisheria na kurahisisha ulipaji kodi.
“Mabadiliko haya yatasaidia kupanua wigo wa kodi na kuweka mazingira bora zaidi ya ulipaji kodi. Pia, yametoa ufafanuzi wa kisheria pale ambapo kulikuwa na utata ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho kwa baadhi ya tarehe za ulipaji kodi,” alisema Bi. Mkumbo.
Baadhi ya wafanyabiashara waliopata fursa ya kuhudhuria semina hiyo walieleza kufurahishwa na elimu waliyopewa, wakisema itawasaidia kutekeleza wajibu wao ipasavyo.
Joseph Kahungwa, mmoja wa wafanyabiashara, alisema kuna mabadiliko yaliyoongeza viwango vya kodi na mengine yaliyopunguza lakini mengi yametoa nafuu hasa kwa biashara ndogo ndogo ambazo sasa zitasajiliwa na kuchangia mapato ya serikali.
Kabla ya semina hiyo, yalitangulia mafunzo ya mabadiliko hayo ya sheria kwa upande wa watumishi wa TRA Mkoa Mwanza ili kuwapa uelewa na kuwasaidia kusimamia utekelezaji wa sheria hizo kwa weledi na ufanisi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza Bw. Faustine Mdessa akifungua semina ya wafanyabiashara kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya TRA mkoani humo.
Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Eugenia Mkumbo akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 katika semina ya wafanyabiashara iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya TRA mkoani Mwanza.

Afisa Mwandamizi Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Isdori Morgan akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 katika semina ya wafanyabiashara iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya TRA mkoani Mwanza.
Baadhi ya Walipakodi waliohudhuria semina ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 wakifuatilia kwa makini semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya TRA mkoani Mwanza
.
Mfanyabiashara wa vipodozi Bw. Valence Samba akitoa maoni yake wakati wa semina ya wafanyabiashara kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya TRA mkoani Mwanza.
Mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza, Bw. Deodatus Sigifrid akichangia hoja wakati wa semina ya wafanyabiashara kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya TRA mkoani Mwanza.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza wakifuatilia kwa makini semina ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya TRA mkoani Mwanza