Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule atembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na kupata maelezo kutoka kwa Meneja wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (MBP), Elizabeth Bolle ya namna Mamlaka inajiridhisha na ubora wa mbolea kuanzia inapoingizwa kutoka nje ya nchi pamoja na kukagua na kupima ubora wa mbolea katika maghala ya kuhifadhia mbolea kabla hazijaingia sokoni kwa matumizi.
Aidha alieza namna huduma hizo zinavyopatikana kupitia ofisi zetu za kanda zote zilizopo nchi nzima.



