![]() |
NA MWANDISHI WETU
KAMISHINA wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Abdul-Razaq Badru ametembelea vikundi vya ujasiriamali kutoka Wilaya za Karatu na Ngorongoro mkoani Arusha ambavyo vimewezeshwa na NCAA kushiriki maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa sabasaba.
Vikundi hivyo vimewezeshwa kushiriki maonyesho hayo ili kuonesha na kuuza bidhaa za kiutamaduni na kiasili kama vile asali, shanga na vinyago kwa wageni mbalimbali wanaotembelea maonyesho hayo jijini Dar es Salaam