Mwandishi Wetu,
Asilimia 100 ya wakazi wa mji wa Njombe wanatarajia kupata huduma ya majisafi ,salama na ya kutosheleza.
Hatua hiyo ni matokeo ya mradi wa maji wa miji 28 unaotekelezwa kwa thamani ya dola za Marekani milioni 15.7.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amekagua mradi huo na kuridhika na utekelezaji wake.
Mhe. Aweso akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amewahakikishia wananchi wa Njombe kuwa changamoto zote walizopitia katika huduma ya maji zinafika mwisho mara baada ya kukamilika mradi huo.
Aidha amemkabidhi Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka nafasi ya kuchukua hatua kwa wakandarasi wote watakaokwamisha malengo ya mradi
Mkuu wa Mkoa Mhe. Mtaka amempongeza Waziri na Menejimenti nzima ya Wizara ya Maji kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ambao ni tumaini kubwa la wananchi.
Amemhakikishia Waziri Aweso kuwa mkoa wa Njombe utaendelea kulinda, kutunza na kuendeleza vyanzo vya maji ikiwemo upandaji miti rafiki wa maji ili kuwezesha uendelevu wa miradi.
Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma Waziri amesema watahakikisha ubora wa miradi ya maji inafikiwa kwa usimamizi makini.
Pia amewahakikishia wananchi kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya "kumtua mama ndoo ya maji kichwani inatimia