Mwandishi Wetu,
Mjumbe wa Bodi, Dkt. Peter Shimo, amepongeza namna TFRA inavyotoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya mbolea na mnyororo wa thamani wa pembejeo hiyo muhimu kwa kilimo chenye tija.
Akiwa katika banda la TFRA, Dkt. Shimo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya taasisi za kilimo chini ya Wizara ya Kilimo katika kuwafikia wakulima na kuongeza ufanisi kwenye sekta hiyo.
Aidha, Dkt. Shimo ameitaka TFRA kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea hasa kuelekea msimu mpya wa kilimo wa mwaka 2025/2026, sambamba na kuvutia wawekezaji kwenye uzalishaji wa mbolea nchini.
Kwa upande wake, Meneja wa Uhusiano, Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa TFRA, Matilda Kasanga, amesema wakulima wengi wamejitokeza kupata elimu na kusajiliwa kwenye mfumo wa pembejeo za ruzuku utakaowawezesha kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali.
Katika ziara hiyo, Dkt. Shimo ametembelea pia mabanda ya TARI @official_taritanzania , TFC na Agrami Afrika, na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha mahusiano kati ya taasisi hizo kwa maslahi ya mkulima na maendeleo ya kilimo nchini.