WANANCHI WA SIHA WARIDHIA DKT. MOLLEL KUENDELEA NA UBUNGE

 Siha, Kilimanjaro

Wananchi wa Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro wamemuidhinisha Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt. Godwin Mollel, kuendelea kugombea nafasi hiyo kwa awamu nyingine.

Tukio hilo limetokea wakati wa hafla ya kimila iliyowakutanisha wanajamii wa Kimaasai wilayani Siha, ambapo Dkt. Mollel aliuliza kwa heshima kama anaweza kuendelea kugombea ubunge wa jimbo hilo, na kupokea ridhaa ya wazi kutoka kwa wananchi waliohudhuria.

Wananchi hao walionesha kuridhishwa na utendaji wa Dkt. Mollel katika kipindi chake cha uongozi, wakieleza kuwa ameleta mageuzi makubwa katika sekta ya afya na maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Dkt. Mollel ameongoza Jimbo la Siha tangu mwaka 2015 na ameendelea kushikilia nafasi ya Naibu Waziri wa Afya, akihusishwa na mafanikio kadhaa katika kuboresha huduma za afya nchini.



Post a Comment

Previous Post Next Post