
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dr Venance Mwasse na Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA(T) Anthony Kasore waliweka saini katika hati ya makubaliano ya kuthibitisha matumizi ya Nishati safi ya Rafiki Briquettes katika vyuo vyote vya Veta.
Katika makubaliano hayo, VETA pia itatengeneza majiko banifu yanayofanya vizuri na Rafiki Briquettes na kuyasambaza katika vyuo vyake lakini pia kwenye taasisi nyingine.
Katika makubaliano hayo VETA wamejitolea kuwapa mafunzo mawakala wanaouza na kusambaza Rafiki Briquettes nchini Wanawake na Samia Nchi Nzima
Hiki ni kishindo kingine cha Serikali ya Awamu ya Sita ambayo moja ya ajenda zake ni kuhakikisha zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia Nishati safi kufikia mwaka 2034