Mwandishi Wetu,
Kilimo kinachozingatia usharuri wa wataalam na kanuni bora za kilimo huleta matokeo chanya kwa mkulima nchini.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Allan Mariki alipotembelea Shamba Darasa la wakulima wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) la Wanyausi lililopo katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Mariki amesema, Mashamba hayo yanaendelea vizuri na kubainisha yametimiza miezi miwili tangu kupandwa kwake ambapo matokeo ya matumizi sahihi ya mbolea yameoneka kutokana na uzaaji wa mahindi kuwa mzuri kwa kuzaaa kuanzia mahindi mawili hadi matatu kwenye mmea mmoja.
Amesema, wanategemea kuanza kuvuna mazao hayo ndani ya wiki ya kwanza ya mwenzi Decemba tayari kwa ajili ya kupelekwa sokoni hususani kwa wale wanaochoma mahindi barabarani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kikundi cha wanyausi, Bw. Michaeli Ngunesi ameishukuru TFRA kwa ushauri wa kitaalam walioutoa kwa wakulima nankupelekea kupata matokeo hayo.
Aidha, ameishukuru kwa kuwezesha upatikani wa Mbolea iliyotumika kwenye mashamba hayo.
Shamba darasa hilo lenye ukubwa wa ekari 20 linatarajiwa kuvunwa kiasi cha tani 50 za mahindi.
