MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA MKUU TRA

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila Leo Septemba 3,2024 amekutana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.Yusuph Mwenda akiongozana na baadhi ya wataalamu wa mamlaka hiyo katika kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala Boma.


Katika kikao hicho Mhe.Chalamila ameongelea mambo kadhaa yaliyojadiliwa ikiwa ni kupunguza migogoro ya kikodi inayolalamikiwa na wafanyabiashara, kutanua wigo wa walipa kodi kulingana na vyanzo vingi vya mapato vilivyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam na pia kuboresha miundombinu ya kikodi ili TRA iweze kukusanya mapato zaidi.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA amemshukuru Mhe Chalamila kwa ushirikiano anaoutoa kwa kufanya kazi na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa wilaya zote tano za Dar es salaam na kuthibitisha kuwa Dar es salaam ni kitovu cha biashara kwa kuwa inakusanya kodi zake zote kwa asilimia takribani 80%.

Mwisho RC Chalamila amepongeza timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuahidi ushirikiano wa kutoka kwa TRA kuhakikisha kodi inakusanywa kwa maendeleo ya Taifa.










Post a Comment

Previous Post Next Post