Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent, amewataka watumishi wa Mamlaka kuwa wabunifu katika kudhibiti mbolea za maji zinazozalishwa kwa kiasi kikubwa Kanda ya Kaskazini.
Ametoa wito huo leo, tarehe 23-02-2023 alipotembelea ofisi ya kanda hiyo na kuzungumza na watumishi.
Pamoja na hilo, Laurent amewataka watumishi hao kudumisha ushirikiano wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
Mwisho Laurent, amewataka watumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja kwa kuzingatia mwongozo wa Mamlaka wa utoaji huduma kwa wateja.
