KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAIPONGEZA WIZARA YA NISHATI KWA KAZI NZURI YA KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME WA SGR.






**Yaishukuru Serikali kwa kutoa fedha kufanikisha Miradi hiyo.*

**Yatoa Rai kwa Serikali kutoa elimu kwa wananchi kuzuia ajali zinazoweza kutokea katika maeneo ya Mradi*

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara  na Taasisi yake ya  TANESCO kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kukamilisha ujenzi wa Mradi wa njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa KV 220 kutoka Kinyerezi (Dar-es-Salaam hadi Kingolwira (Morogoro) yenye urefu wa Kilomita 160 ambayo itakuwa na umeme wa uhakika utakaolisha vituo vyote vinne vya kupoza umeme vilivyopo katika reli ya kisasa.

Pongezi hizo zimetolewa tarehe 11 Novemba, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dkt. David Mathayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa KV 220 kutoka Kinyerezi (Dar-es-Salaam hadi Kingolwira (Morogoro) kwa ajili ya uendeshaji wa Treni ya Mwendokasi na kukamilisha  kazi hiyo kwa asilimia mia moja.

Kamati hiyo pia , imetembelea Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Msamvu na kuelezea kufurahishwa kwake na utayari wa Kituo hicho kuhudumia miundombinu kwa ajili ya treni ya Mwendokasi (SGR).

Akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dkt. David Mathayo  ameiomba Serikali kutoa elimu kwa Wananchi walio jirani na maeneo ya Mradi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

"Ninamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia  Suluhu Hasan ,kwa kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha Mradi wa Miundombinu ya Mradi wa SGR.. Pia tumejionea wenyewe Mradi wa Umeme kutoka Kinyerezi mpaka Msamvu umekamilika kwa asilimia mia moja.Kamati tumeridhishwa sana na Mradi ambao Serikali imefanya." Amesema Mwenyekiti huyo.

Dkt. Mthayo amesisitiza kuwa maeneo ambayo Treni ya Umeme imepita ni vyema Serikali kuongeza ulinzi kwa kushirikiana na Serikali za  Mitaa kuhakikisha  Wananchi hawapiti katika maeneo yaliyowekewa uzio ili kuzuia ajali ambazo zinaweza kutokea

Dkt. Mathayo amelihimiza  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  kukamilisha kazi katika maeneo machache  yaliyobakia ambayo ni asimia moja kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili kukamilisha mambo yaliyobakia.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema Wizara ya Nishati itaongeza usimamizi kuhakiksha Mradi unakamilka kwa Wakati kwa maeneo yaliyosalia.


*MAELEZO YA PICHA*

*PICHA Na.1*


*PICHA Na .2*

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. David Mathayo (kushoto) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (wa pili kutoka kushoto) wakipata Maelezo kuhusu Mradi wa njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa 220 kV kwa ajili ya Uendeshaji wa Treni ya Umeme ya Mwendo Kasi (SGR) mara baada ya Kamati hiyo kutembelea Kituo hicho tarehe 11 Novemba, 2023.

*PICHA Na 3*

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. David Mathayo, wakitembelea kituo cha Kupokea na kupoza Umeme cha Kingolwira cha Mradi wa njia ya  Kusafirisha Umeme wa Msongo wa 220 kV kwa ajili ya Uendeshaji wa  Treni ya  Mwendo Kasi (SGR) wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara yake ya kawaida ya kikazi Mkoani Morogoro tarehe 11 Novemba, 2023.

*PICHA Na.4*

Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Nishati na Madini ikiongozwa na Mwenyekiti wa  Kamati hiyo Mhe. Dkt. David Mathayo (aliye katikati) akiwa pamoja na Naibu  Waziri wa Nishati  Mhe. Judith Kapinga (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa mitambo  ya kupoza umeme kituoni hapo jinsi inavyofanya kazi wakati Kamati hiyo ilipotembelea kituo hicho kilichopo Mkoani Morogoro tarehe 11 Novemba, 2023.

*PICHA Na. 5*

Mwenyekiti wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dkt. David Mathayo akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoani Morogoro wakati Kamati hiyo ilipotembelea kituo hicho kilichopo Mkoani Morogoro tarehe 11 Novemba, 2023 kushoto kwake, ni Naibu Waziri wa Nishati  Mhe. Judith Kapinga.

*PICHA Na.6*

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea kituo cha Kupokea, Kupoza na kusambaza Umeme cha Msamvu wakati Kamati hiyo ilipotembelea kituo hicho tarehe 11 Novemba, 2023.

*PICHA Na.7*

Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Nishati na Madini ikiongozwa na Mwenyekiti wa  Kamati hiyo Mhe. Dkt. David Mathayo (wa kwanza kushoto) akiwa na Naibu  Waziri wa Nishati  Mhe. Judith Kapinga (wa pili kutoka kulia kwake) baada ya kutembelea Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza Umeme cha Msamvu wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara yake ya kikazi ya kawaida Mkoani Morogoro tarehe 11 Novemba, 2023.

Post a Comment

Previous Post Next Post