Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nundu akiwa katika Kongamano la 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu leo tarehe 15/6/2023 linalofanyika kwa siku tatu kuanzia Juni 14- 16, 2023 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Cha Kumbukumbu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Teknolojia, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Erasto Mlyuka (kulia) akichangia mada leo tarehe 15/6/2023 katika kongamano la 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu linalofanyika kwa siku tatu kuanzia Juni 14- 16, 2023 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Cha Kumbukumbu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu leo tarehe 15/6/2023 linalofanyika kwa siku tatu kuanzia Juni 14- 16, 2023 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Cha Kumbukumbu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeendelea kutekeleza mipango ya kuwasaidia wanafunzi waliobuni miradi ya kisayansi ambayo inakwenda kutatua changamoto katika jamii.
Akichangia mada leo tarehe 15/6/2023 katika Kongamano 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
Dkt. Amos Nundu, amesema kuna programu mbalimbali wamekuwa wakifanya katika kuhakikisha wanawasaidia vijana ambao wamebuni miradi ya kisayansi.
Dkt. Nundu amesema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kusaidia miradi yenye tija katika jamii ambayo inakwenda kusaidia katika kufikia malengo ambayo yamekusudiwa.
“Waliobuni miradi ya kisayansi yenye faida tumekuwa tukiwasaidia kuwaunganisha na taasisi mbalimbali kwa ajili kufanya nao kazi na kuendeleza mradi wake” amesema Dkt. Nundu.