NAIBU WAZIRI MASANJA AONGOZA KIKAO CHA TAASISI ZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII





Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja  ameongoza kikao cha kimkakati cha  kufanya mapitio ya taarifa mbalimbali za utendaji kazi  za Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na hatimaye kukuza utalii na kuimarisha usimamizi wa Uhifadhi wa Maliasili nchini.

Kikao hicho kimefanyika leo Machi 6, 2023 katika Ukumbi wa  Ofisi za Ngorongoro zilizopo Jijini Arusha.

Mhe.Masanja ametumia fursa hiyo kuwataka watendaji wa Taasisi  kuwa wabunifu kwa kutumia historia ya taifa na elimu ya viumbe hai kuwa fursa ya kujifunza na kuiongezea Serikali Mapato na kuongeza ajira na kipato kwa Mwananchi mmoja mmoja.

Aidha, kikao hicho  kilijadili namna ya kutumia Makumbusho za Taifa kama eneo mojawapo la kuiongezea Serikali mapato kwa kuwa wana wigo mpana zaidi kuliko Taasisi nyingine katika kuibua fursa zilizopo nchini.

Katika hatua nyingine, Mhe.Masanja  amekielekeza Chuo cha FITI kuandaa mpango utakaokiwezesha Chuo hicho kuwepo na miradi mbalimbali itakayokiwezesha  kuongeza mapato kwa njia  ya Mafunzo.

Taasisi zilizoshiriki kikao hicho ni Shirika la Hifadhi za Taifa  (TANAPA) Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA),  Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI), Makumbusho ya Taifa ( NMT)  pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

Post a Comment

Previous Post Next Post