Waziri wa Nishati January Makamba akihutubia Wakandarasi, Wajumbe wa Bodi Nishati Vijijni (REB) na Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijijni (REA) kwenye hafla ya utiaji saini Mikataba ya Utekelezaji wa Mradi wa Kupeleka Umeme katika Maeneo ya Pembezoni mwa Miji Awamu ya Tatu (PERI Urban III) kati ya REA na Wakandarasi katika ukumbi wa JNICC, Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nishati January Makamba akihutubia Washiriki katika hafla ya utiaji saini Mikataba ya Utekelezaji wa Mradi wa Kupeleka Umeme katika Maeneo ya Pembezoni mwa Miji Awamu ya Tatu (PERI Urban III) kati ya REA na Wakandarasi katika ukumbi wa JNICC, Jijini Dar es Salaam
Wakandarasi wakimsikiliza Waziri wa Nishati January Makamba wakati akihutubia kwenye hafla ya utiaji saini Mikataba ya Utekelezaji wa Mradi wa kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wakandarasi katika ukumbi wa JNICC, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy akipena mkono na Mwakilishi wa Kampuni ya Central Electricals International Ltd Bwana Akbar Meghji mara baada ya kusaini Mkataba wa Kupeleka Umeme katika Maeneo ya Pembezoni mwa Miji Awamu ya Tatu (PERI Urban III) katika mkoa wa Singida.
Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia utiaji saini mikataba ya Kupeleka Umeme katika Maeneo ya Pembezoni mwa Miji Awamu ya Tatu (PERI Urban III) kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy na Mwakilishi wa Kampuni ya DERM Bi. Bridget Temba katika ukumbi wa JNICC, Jijini Dar es Salaam
…………………………………..
WAZIRI January Makamba amesema kuanzia sasa Wakandarasi wa Miradi ya kupeleka umeme vijijini watapimwa kwa utendaji wao (Performance) na si vinginevyo na kuongeza kuwa Wakandarasi ambao utendaji wao ni wa mashaka, wasahau kupata zabuni za Miradi ya REA.
Waziri Makamba ameyasema hayo leo mchana tarehe 19 Disemba, 2022 na amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini (REA); Mhandisi Hassan Saidy kutosaini mikataba miwili na Kampuni ya ETDCo kutokana na utendandaji usiolidhisha.
Katika maelezo yake; Waziri Makamba amesema Kampuni ya ETDCo imeonyesha udhaifu mkubwa kwenye utekelezaji wa miradi kadhaa ya kupeleka nishati vijijini ambapo ametoa mfano kwenye mkoa wa Mbeya; Kampuni hiyo kwenye mradi mmoja imefanya kazi kwa asilimi 28 tu hadi sasa.
“ETDCo leo hakuna kusaini mkataba wa Mradi wa PERI Urban III, nendeni kwanza mkakamilishe kazi mkoani Mbeya na Katavi, nimeona kwenye Mradi wa PERI Urban mmeshinda zabuni ya mkoa wa Kigoma na Geita na kazi zote hizo zina thamani ya shilingi bilioni 18.”
“Hii si sawa na mmeshindwa kutekeleza miradi kwa wakati, mfano mkoani Katavi kwa kazi ile mlitakiwa hadi sasa walau mngekuwa mmefika asilimia 81 ya utekelezaji lakini bado utekelezaji upo chini.” Amesisitiza Waziri Makamba.
Wakati huo huo, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imesaini Mkataba wa PERI Ubani Awamu ya Tatu. Mradi huo una lengo la kupeleka umeme katika maeneo ya pembezoni mwa miji. Mikoa ambayo imelengwa ni pamoja na Geita, Mtwara, Mbeya, Tabora, Tanga Singida, Kigoma ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA); Mhandisi Hassan Saidy alisaini mikataba kwa niaba ya Serikali na Watendaji wa Kampuni nne katika ukumbi wa Mikumi katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Julius Nyarere, Jijini Dar es Salaam.
Kampuni hizo ni pamoja na Central Electricals International Ltd, DERM Electrics (T) Ltd, OK Electrical & Electronics Services Ltd na DIEYNEM Co Ltd.