Waziri wa Nishati Januari Makamba(wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la kuanza kujaza maji katika bwawa la Julius Nyerere(JNHPP) lililopo Rufiji mkoani Pwani.Tukio hilo la kuanza kujaza maji linatarajiwa kufanyika Desemba 22 mwaka huu ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Kulia kwenye picha hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Maharage Chande na kushoto ni viongozi kutoka Wizara ya Nishati.Baadhi ya wakandarasi wa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere wakiwa kwenye kikao cha Waziri wa Nishati Januari Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kujazwa maji kwa bwawa hilo tukio ambalo litafanyika Desemba 22 mwaka huu.Muonekano wa handaki la kuchepusha maji kama ambavyo linaonekana baada ya ujenzi wake kufikia asilimia 78.68.Waziri wa Nishati Januari Makamba akijadiliana jambo na maofisa wa TANESCO pamoja na Wizara ya Nishati leo Desemba 18 mwaka 2022 baada ya kutangaza rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la kubonyeza kitufe kuashiria kuanza ujazwaji wa maji kwenye bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere lililpo Rufiji mkoani Pwani.
......................................
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio la kushuhudia ufungaji wa lango la handaki mchepuko (diversion tunnel) ili kuruhusu maji kuanza kujaa katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere litakalofanyika siku ya Alhamis, Tarehe 22 Disemba 2022
Akizungumza na waandishi wa Habari katika eneo la mradi wa umeme wa Mto Rufiji Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amesema mradi huo unahatua kubwa mbili ambazo Zina hadhi ya kushuhudiwa na kusherehekewa ambapo hatua ya kwanza ni kufunga lango la njia ya mchepusho wa maji na ya pili ni kuwasha mitambo ya kufua umeme
“Kwa ujumla hadi Leo mradi huu umefikia hatua ya asilimia 78, ni hatua kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na katika hatua za mradi, mradi huu unaa maisha na Kuna Alama ambazo tunafikia siku zote na hatua zote ni muhimu. Tumemaliza kujenga tuta, barabara, tumemaliza kujenga nyumba za wafanyakazi kwahiyo Kuna mafanikio katika kipindi chote, sasa tumefikia kwenye mafanikio makubwa tangu tuanze ujenzi wa mradi huu na yenyewe ni kujaza maji kwenye bwawa , kazi ya kujenga handaki la kuchepusha maji ilifanyika miaka mitatu iliyopita na handaki Hilo Lina urefu wa mita 700 na ujenzi uligharimu sh bil 235
Mhe. Makamba amesema kuwa kutokana na umuhimu wa hatua hiyo ya mradi ulipofikia hatua hii ya kuanza kujaza maji kwenye bwawa itazinduliwa na na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Tar 22 Disemba 2022 siku ya Alhamisi ambapo Mheshimiwa Rais atabonyeza kitufe ambacho kitashusha geti la kuziba handaki lilikuwa linachepusha maji na rasmi maji yataanza kujaa kwenye bwawa
Ameongeza kuwa Shughuli hiyo itauzuliwa na watu takribani 2000 wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na viongozi wengine kama spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mawaziri, Makatibu Wakuu, wakuu wa Mikoa na Wilaya zinazozunguka Bonde la mto Rufiji, viongozi wa Dini, Viongozi wa Chama na wananchi, lakini pia serikali ya Misri ambapo ndipo wanatoka wakandarasi wanaojenga mradi huo, mawaziri, viongozi we serikali pamoja na vyombo vya Habari vya nchi hiyo watahudhuria wakiongozwa na waziri wa mambo ya nje nchini Misri.
Akizungumzia faida za mradi huo Mh. Makamba amesema ndani ya Serikali mradi huu ni mpana zaidi na utasaidia pia katika masuala ya Kilimo chini ya mto Rufiji, Uvuvi, Kuondoa mafuriko, Upatikanaji wa huduma za maji wa uhakika kwa Jiji la Dar es Salaam, Utalii, miundombinu na usafirishaji pamoja na kupata umeme wa uhakika.
Naye Mkurugenzi wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Maharage Chande ameeleza kuwa inakadiriwa kwamba misimu miwili ya mvua itaweza kufanya bwawa Hilo la Julius Nyerere kujaa maji hivyo zinatazamiwa mvua za masika Machi 2023 na 2024 kuweza kujaza Bwawa hilo.
Mradi wa kufua umeme kwa njia ya maji wa Julias Nyerere amamba unakadiriwa kuzalisha megawati 2115, ulianza kujengwa mwaka 2019 na unatarajiwa kukamilika June 2024 na umegharimu kiasi cha Shilingi Trilion 6.5 ukiwa umebakisha asilimia 22 mpaka kukamilika