KITUO CHA KUPOZA UMEME IFAKARA CHAFIKIA ASILIMIA 80,KUKAMILIKA MACHI 2023

   



MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Seif Saidy, akizungumza na waandishi wa habari Ifakara Morogoro (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ifakara na Kilomita 82 za miundombinu ya usambazaji wa umeme katika Wilaya ya Kilombero na Ulanga.



BAADHI ya Waandishi wa habari Wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Seif Saidy,wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ifakara na Kilomita 82 za miundombinu ya usambazaji wa umeme katika Wilaya ya Kilombero na Ulanga.



KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Rodney Thadeus,akiipongeza
REA kwa kuzidi kuboresha huduma za Nishati kwani huduma nyingi zinategemea umeme
 

MAFUNDI wakiendelea na Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ifakara ambapo umefikia asilimia 80.1 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2023

 
MUONEKANO wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ifakara ambapo umefikia asilimia 80.1 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2023

....................................

Na Alex Sonna-IFAKARA,MOROGORO

MRADI wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ifakara umefikia asilimia 80.1 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2023 ambapo mpaka sasa tayari transfoma ya kisasa imeshawekwa na kituo kitatoa njia nne za umeme ambazo zitapeleka umeme kwenye maeneo mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Seif Saidy wakati akizungumza na waandishi wa habari Ifakara Morogoro kuhusu kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kituo hicho na Kilomita 82 za miundombinu ya usambazaji wa umeme katika Wilaya ya Kilombero na Ulanga.


Mhandisi Saidy amesema kuwa mradi umefikia asilimia 80.1 ya ujenzi wake na ulianza kujengwa Machi 2020 na unategemewa kukamilika Machi 2023

''Mradi huu wa kupoza umeme Ifakara utawezesha kupatikana kwa umeme wa kutosha masaa yote, kukomesha kukatika umeme mara kwa mara na kuondoa kero ya kuungua kwa vifaa na mitambo ya umeme.''amesema Mhandisi Saidy


Pia ameema kuwa mradi huo unatarajiwa kuhudumia Wananchi takriban 100,000 wa wilaya za Kilombero na Ulanga.






Post a Comment

Previous Post Next Post