NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII AIPONGEZA TTB

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Juma Mkomi akikagua kazi zilizofanyika upitia Fedha za UVIKO 19Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Felix John akitoa maelezo kuhusu mipango, mafanikio na changamoto za Bodi wakati wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Menejimenri ya TTB.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Juma Mkomi akisikiliza maelezo kuhusu kazi zinazofanyika katika Kituo cha Kutolea Taarifa za Utalii Kidijitali.Picha ya pamoja, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Juma Mkomi na Menejimenti ya Bodi ya Utalii Tanzania.

************************

Naibu Katibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Juma Mkomi ameipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kazi nzuri iliyofanyika kupitia fedha za UVIKO 19 ambapo TTB ni moja ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyonufaika na fedha hizo.

Pongezi hizo amezitoa wakati wa ziara yake yenye lengo la kukagua matumizi ya shughuli zilizopangwa kufanywa na TTB kupitia fedha za uviko -19. Katika Ziara hiyo ameweza kupata taarifa ya matumizi ya fedha na kujionea kazi zilizofanywa ikiwa ni pamoja na manunuzi ya vifaa vya Kituo cha Kutoa Taarifa za Utalii Kidijitali (Digital Marketing Command Centre).

“TTB ilipata kiasi cha shilingi bilioni 10, imeweza kukamilisha Mradi wa Kituo cha kutoa taarifa za utalii wa Tanzania kidijitali, ambapo vivutio vyote vya Tanzania vitaweza kutangazwa kidijitali na kufikia masoko yote ya utalii duniani pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya utalii ili kuweza kuwavutia wawekezaji wengi. Amesema Bw. Mkomi.

Ameongeza kuwa, kazi kubwa imeshafanyika hivyo nimeielekeza TTB kushirikiana na Taasisi nyingine zenye dhamana ya kusimamia maeneo ya vivutio vya utalii  ili kuweza kupata taarifa sahihi na kuzitangaza. Aidha, vifaa vya kisasa vya kutayarisha taarifa; picha za mnato na video vipo, tunahitaji kuongeza nguvu za wataalamu zaidi ili kuweza kufikia lengo tulilojiwekea.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Felix john ametumia fursa ya ziara hiyo kueleza Mikakati ya TTB ya Utangazaji , Mafanikio na changamoto zilizopo katika kutekeza shughuli nzima za kutangaza utalii wa Tanzania

Post a Comment

Previous Post Next Post