TRA ILALA YAWAKUMBUKA WENYE MAHITAJI MAALUM KITUO CHA MISSIONARY CHARITY

Kaimu Meneja wa Kikodi Mkoa wa Ilala Masau  Malima akizungumza na waandishi wa habari kuelezea dhamira yao ya kwenda kutoa zawadi katika kituo cha watu wenye Mahitaji Maalum cha Missionary Charity Nyumba ya amani na furaha
Mmoja ya wazee katika kitua hicho Joachim Michael akitoa shukrani Kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)Mkoa wa Kikodi Ilala baada ya kuwapatia msaada wa vitu Mbalimbali
Baadhi ya bidhaa zilizotolewa katika kituo hicho cha Missionary Charity Nyumba ya amani na furaha 
Kaimu Meneja Mkoa wa Kikodi Ilala Masau  Malima akimkabidhi zawadi Mzee Joachim Michael kutoka kituo cha watu wenye Mahitaji Maalum cha Missionary Charity zawadi ikiwa ni muendelezo wa siku ya kipindi cha huduma na shukrani kwa mlipa kodi.
Kaimu Meneja Mkoa wa Kikodi Ilala Masau  Malima akimkabidhi Mzee Joachim Michael kutoka kituo cha watu wenye Mahitaji Maalum cha Missionary Charity Nyumba ya amani na furaha sehemu ya zawadi katika muendelezo wa siku ya kipindi cha huduma na shukrani kwa mlipa kodi.
........................................

Mwandishi Wetu
KAIMU Meneja wa Kikodi Mkoa wa Ilala, Masau Malima amesema kwa mwaka huu wa fedha wana lengo la kukusanya Trilioni 1.25 kutokana na ushirikiano wanaupata kutoka kwenye makundi mbalimbali ya walipa kodi.

Malima alisema hayo jana baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwenye Kituo cha watu wenye mahitaji maalum cha Missionary Charity kilichopo Mburahati, Dar es Salaam katika muendelezo wa kipindi cha huduma na shukrani kwa mlipa kodi.

Alisema wao kama mkoa wa kikodi wa Ilala wanaendelea kufanya shughuli zao za kukusanya mapato hadi kufikia mwezi wa Oktoba mwaka huu ufanisi wao ulikuwa ni wa asilimia 104.5 katika lengo ambalo walikuwa wamepangiwa. 

Malima alisema mkoa wao umeendelea kuonesha ustaimilivu katika ukusanyaji wa mapato, ambapo hadi sasa ukuaji wao wa makusanyo upo zaidi ya asilimi 25 ukilinganisha na mwaka uliopita.

"Kama unavyokumbuka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  kutokea Novemba 13, mwaka huu tulianza kuanzimisha siku ya shukrani kwa mlipa kodi, kipindi 
hiki kinaendelea hadi  Novemba 30,2022,"

"Tumekuja hapa kuleta zawadi mbalimbali na shukrani lengo likiwa  ziweze kusaidia katika shughuli zinazoendelea hapa sisi kama sehemu ya jamii tumeguswa sana na makundi haya," alisema Malima 

Pia, Malima alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan na baraza lake la mawaziri kwa miongozo mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa hasa katika Taasisi yao.

Kwa upande wake, Mzee Joachim Mkila alisema anamiaka karibu tisa katika kituo hicho, ambapo wamepokea msaada kwa mikono miwili ingawa na watu wengine wanaleta lakini aliyetoa katoa.

"Tunashukuru sana kwa zawadi hizi mmetusaidia kwa kila kitu, hapa hakiuzwi kitu,kikiingia kimeingia, hapa tupo wengi ukihesabu sahani hata 100 zinafika tunaomba na watu wengine kutoa msaada kama huu,"alisema  Mkila.

Post a Comment

Previous Post Next Post