Waziri Mchengerwa atoa siku 30 kwa BMT kutengeneza mifumo ya kusajili ya kielektoniki

Na John Mapepele 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakiksha ndani ya mwezi mmoja linatengeneza mfumo wa kieletroniki wa kusajili vyama vya michezo ili kuondoa usumbufu kwa wadau unaojitokeza.

Mhe. Mchengerwa ameyasema  haya  leo Oktoba 27, 2022 wakati akizindua program ya “Mpira Fursa” inayoratibiwa na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO) na kugawa  vifaa vya michezo kwa  Vyuo vya Wananchi vya  Maendeleo 54 kote nchini na shule za msingi 86.  

Ameutaka uongozo wa shule ambazo zitabahatika kupata vifaa vya soka, kuwaruhusu wasichana kucheza soka na kuvitumia vifaa hivyo kwa uangalifu na kwa madhumuni yaliyokusudiwa.  

Ameipongeza KTO kwa kuanzisha program hiyo ya kupeleka  michezo  katika vyuo vya  wananchi  vya maendeleo na shule za msingi huku akifafanua kuwa  huo ni utekelezaji wa  maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan   ya kwenda mtaa kwa mtaa ya kusaka vipaji vya michezo na Sanaa.

 “Naomba niwaeleze ninyi mnatafsiri nini rais anataka kufanya kwa watanzania kwenye sekta za michezo, hususan utekelezaji wa program ya Mtaa kwa Mtaa, hongereni sana” amepongeza Mhe. Mchengerwa 

Amesema ukiboresha sekta ya michezo utapunguza gharama za maeneo mengine kama afya na utalii, na amewashauri wadau kuwekeza kwenye sekta ya michezo ambapo amesema wakati ni sasa ambapo Mhe. Rais anatoa msukumo  mkubwa kwenye sekta za michezo.

Aidha, amewataka Watendaji wa Sekta za Michezo kujipanga vizuri na kuwa  na mkakati madhubuti utakaosaidia kufanya maandalizi kabambe ya kushiriki kwenye  kombe  la dunia  mwaka 2030.

Amehoji kuwa Tanzania ina zaidi ya watu milioni sitini  kwa nini inashindikana kufanya vizuri, wakati kuna  miundombinu  bora ya  michezo  huku akitolea mfano wa Uwanja wa Mkapa kuwa una sifa za kimataifa.  Ameongeza kuwa kama timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 imeweza kuwatoa mabingwa wa soka kama Ufaransa na Canada,inakuwaje  timu za soka  kwa wanaume zinashindwa kufanya  vizuri.



 

Post a Comment

Previous Post Next Post