TRA MKOA WA MBEYA YASEMA KUNA ONGEZEKO LA ULIPAJI KODI KWA HIYARI KATIKA SEKTA YA KILIMO

 MAMLAKA ya Mapato mkoa Mbeya (TRA) imesema kuwa kumekuwa na ongozeko  la ulipaji kodi kwa hiyari hasa upande wa kilimo kutokana na kutatua migogoro nje ya Mahakama.

Imesema kuwa mikakati iliyowekwa kwa mlipa kodi kipindi hiki cha Maonyesho ya wakulima Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika jijini mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani  humo Agosti,6, nwaka huu  Kaimu Meneja wa Mamlaka ya mapato  Mkoa wa Mbeya(TRA)Nuhu Suleiman amesema mikakati waliyoweka kwa walipa kodi katika kipindi hiki cha maonyesho ya wakulima Nanenane inatija hususani kwa wakulima. 

Suleiman amesema kuwa kitu kingine kinacholeta msukumo wa hiyari kwenye ulipaji kodi ni usikilizaji wa malalamiko kwa walipa kodi ambapo Mamlaka hiyo imejipanga vizuri sana kwa ajili ya kuleta tija.

"Ni kweli suala la kodi linahusu kila mwananchi na wakati mwingine kuna kuwa na changamoto ya nguvu kazi lakini sasa hivi tunaishukuru serikali na pia tunashukuru Serikali yetu inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassan .

Nakuongeza " Ili kuleta tija na ufanisi wa Kikodi Mamlaka  tumeongozewa watumishi 2000 hivyo sisi Kama watumishi tumejipanga kwenda maeneo ambayo yamejitenga na mji kwa ajili kusambaza elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi. "amesema

Mamlaka ya Mapato jiji la Mbeya imejikita kwenye Maonyesho ya kitaifa  Ambayo yanafanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale kwa lengo la kuendelea kuwapa huduma wananchi.

Amesema kuwa hiyo nifursa kwa wawekezaji kuweza kuelewa ni bidhaa gani na vifaa gani ambavyo vinatumika kwenye Kilimo na ambavyo vinamsamaha wa kodi  kuna bidhaa kama mbolea, vyumba vya Barid, chumba vya kukuzia mimea hizo zote ni fursa kwa wawekezaji. 

Ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa waelewe umuhimu wa kulipa kodi kwahiyo wanashukuru sasahivi kumekuwa na ulipaji kodi kwa hiari na kubwa Mamlaka inajitahidi kuzimaliza Kero za wananchi kwenye eneo hilo la Kikodi.

"Tunawashauri wananchi hususani wa mikoa hii ya nyanda za juu kusini kufika kwenye viwanja vya nanenane ili kuja kupata elimu ya kodi na faida zake na kubwa zaidi Rais Samia Suluhu amefanya kazi kubwa ya kutuongezea nguvu kazi. " amesema.

Maofisa wa TRA wakitoa huduma kwa wateja waliotembelea banda lao kwenye Maonyesho ya kitaifa ya Nanenane jijini Mbeya

Post a Comment

Previous Post Next Post