MISAMAHA YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI NI NEEMA KWA WAKULIMA, WAFUGAJI, WAVUVI

 MABADILIKO ya sheria kwa 2022/2023 za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa neema kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kuondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye bidhaa wanazozitumia.


Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Muandamizi wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Lameck Ndinda wakati akitoa tathmini wa ushiriki wa TRA katika maonesho ya nanenane yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mwakangale jijini Mbeya. Amesema kuwa

Misamaha hiyo ni katika bidhaa za kilimo ni matrekta na Vifaa vya Kupima Unyevu nyevu wa Udongo, Vifungashio vya maziwa na Nyavu za kuvulia Samaki.

Amesema kuwa bidhaa hizo zinapoingizwa nchini kutoka Nchi nyingine bidhaa hizo hazitozwi kodi ya Ongezeko la thamani kama bidhaa nyingine.

Amesema kuwa misamaha ya kodi ya ongezeko la thamani imetoa fursa kwa wananchi kujifunza lakini pia wananchi kuuliza maswali ya namna wanavyotoza kodi kwenye shughuli za kilimo, Uvuvi na ufugaji.

Ndinda amesema kuwa katika Maonesho hayo walitoa Elimu juu ya matumizi ya lisiti za EFD na tiketi za VEFD ambazo zitawawezesha wafanyabiashara wa bidhaa kilimo, ufugaji na Uvuvi ambao ni wafanya biashara wadogo kuweka stamp za kieletroniki kwenye mazao yao.

Ndinda amesema kuwa Kama Mkulima, Mfugaji na Mvuvi katika shughuli zake anapata zaidi ya shilingi laki nne kwa mwaka anatatakiwa kisajiliwa TRA ili kupata utaratibu unaoweza kuchangia pato la Taifa.

Amesema kuwa TRA imeongeza nguvu kutoa elimu katika sekta ya kilimo, Uvuvi na Ufugaji ili kuzidi kuwasisitiza wananchi kutumia huduma za kimtandao kwa kutumia simu zao.

"Tumewaelekeza namna ya kufile zile Retun kila mwezi.

"Kwa wale wakulima ambao wanasafirisha mazao yao kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine walikuwa wanapata shida kutoa risiti sasa bidhaa mpya ya TRA ya VEFD itawawezesha wafanyabiashara hizo kuondokana na usumbufu barabarani." Amesema Ndinda
Afisa Mwandamizi wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Lameck Ndinda akitoa tathmini wa ushiriki wa TRA katika maonesho ya nanenane Mbeya.

Post a Comment

Previous Post Next Post