PROF.SEDOYEKA AKUTANA NA MENEJIMENTI YA NCAA NA KUHIMIZA UIMARISHAJI HUDUMA ZA UTALII



 Na Kassim Nyaki, NCAA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Eliamani Sedoyeka tarehe 26 Julai, 2022 amefanya ziara katika ofisi za NCAA Karatu Mkoani Arusha kwa lengo la kukutana na Menejimenti kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha utendaji kazi.

Prof. Sedoyeka ameeleza kuwa kufuatia ongezeko la wageni ni muhimu kuhakikisha kuwa mda wote mitambo inakuwepo barabarani kwa ajili ya kurekebisha sehemu korofi ili kuboresha mawasiliano ya barabara kwa wageni mda wote.

“Kwa sasa Ngorongoro ni moja ya maeneo yanayotembelewa na wageni wengi, Utaratibu mliouanza wa kuweka mitambo ya kurekebisha sehemu korofi uendelee ili kuhakikisha barabara katika maeneo ya Hifadhi zinakuwa bora mda wote”

Ameupongeza uongozi wa NCAA kwa jitihada za kutangaza utalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dkt. Christopher Timbuka amemueleza katibu Mkuu kuwa mkakati wa Mamlaka ni kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea hifadhi kutoka wageni 700,000 waliotembelea Hifadhi mwaka 2018/2019 kabla ya athari ya ugonjwa wa UVIKO-19 hadi kufikia idadi ya wageni 1, 200,000 ifikapo mwaka 2025.

Post a Comment

Previous Post Next Post