Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewatakia heri ya sikukuu ya Idd waislam na watanzania wote.
Salam hizo amezitoa leo Julai 10, 2022 wakati wa swala na baraza la Eid El - Adh'haa kitaifa lililofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Msikiti wa Mfalme wa Morocco Muhammad VI Bakwata Makao Makuu.
Mhe. Mchengerwa amewata watanzania kusherehekea kwa amani na utulivu huku wakimtanguliza Mwenyezi Mungu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Kassim Majaliwa. Majaliwa ndiye mgeni rasmi.
Amesema siku hii ni ya upendo kwa watu wote na ambapo inatakiwa kusherehekewa kwa upendo, amani na mshikamano.
Amewapongeza viongozi wa dini na vyombo vya habari kulielezea zoezi la sensa ya watu na makazi na kuwataka wananchi wote kushiriki.
Aidha, amepongeza taasisi za dini kuendelea kutoa huduma mbalimbali za afya na maji.
Pia Mhe. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa suala la uhamaji wa hiari wa wananchi wa Ngorongoro na uwekaji mipaka eneo la Loliondo.
Amesisitiza kuwa mazoezi haya yanatelekezwa kwa amani na kwa faida kubwa ya taifa letu kwa ujumla
Amesema Serikali kupitia wizara ya Maliasili na inatarajia kuwapeleka viongozi wa dini katika maeneo haya ili kujionea kinachiendelea.
Akimkaribisha Mhe. Waziri Mkuu, Mhe. Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania. Dkt, Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana amewasisitiza waislam wote nchini kujitokeza kwenye zoezi la kuandikishwa kwenye Sensa itakayofanyika Agosti 23, 2022.
Katika tukio hili Makamo Mwenyekiti wa CCM Komrade Abdurahaman Kinana, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mhe, Abdalah Ulega na viongozi mbalimbali wamehudhuria.